RC Mtaka: Wananchi msiwarekodi wataalam wa afya na kupeleka mtandaoni

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amepiga marufuku wananchi kuwarekodi madaktari na kusambaza video au sauti mitandaoni badala yake waweze kutumia njia sahihi ya kutoa taarifa kwa uongozi madaktari wanapokosea.

RC Mtaka ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ukalawa wilayani Njombe baada ya kuzindua kituo kipya cha afya kilichojengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 300 fedha ambayo ni kutoka serikali kuu, mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe pamoja na nguvu za wananchi.

"Wananchi kuweni na lugha nzuri kwa watoa huduma, ujue kwamba nesi anapokuhudumia pengine wewe ni mtu wa ishirini, sitarajii kuona mwananchi ameenda kuzungumza na mtoa huduma amemrekodi na kupeleka mtandaoni", amesema Mtaka na kuongeza,

"Utaongea na nesi utamrekodi na kupeleka mitandaoni akatukanwa halafu kesho utapata shida na kurudi, mimi niwaombe kama kuna changamoto yoyote nenda kwa viongozi wake waambie lugha hii imenikwaza na mengine tuvumiliane"

Chanzo: Jambo
 
Hakika siyo busara ku record na kusambaza mtandaoni
 
Kazi waliyoiomba waitekeleze kulingana na kanuni zao. Warejee kile walichofunzwa na kutambua wanaongea na wagonjwa, sio kumkaripia ama kutoa lugha chafu kwa mgonjwa
 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amepiga marufuku wananchi kuwarekodi madaktari na kusambaza video au sauti mitandaoni badala yake waweze kutumia njia sahihi ya kutoa taarifa kwa uongozi madaktari wanapokosea.

RC Mtaka ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Ukalawa wilayani Njombe baada ya kuzindua kituo kipya cha afya kilichojengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi milioni 300 fedha ambayo ni kutoka serikali kuu, mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe pamoja na nguvu za wananchi.

"Wananchi kuweni na lugha nzuri kwa watoa huduma, ujue kwamba nesi anapokuhudumia pengine wewe ni mtu wa ishirini, sitarajii kuona mwananchi ameenda kuzungumza na mtoa huduma amemrekodi na kupeleka mtandaoni", amesema Mtaka na kuongeza,

"Utaongea na nesi utamrekodi na kupeleka mitandaoni akatukanwa halafu kesho utapata shida na kurudi, mimi niwaombe kama kuna changamoto yoyote nenda kwa viongozi wake waambie lugha hii imenikwaza na mengine tuvumiliane"

Chanzo: Jambo
Mtaka umechoka siyo? Kaombe kupumzika. Unataka uovu ufichwe? We unawajua manesi kweli?
 
Back
Top Bottom