Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuona umuhimu wa kuendesha mafunzo hayo na ni wazi kuwa mafunzo hayo yataongeza uelewa na tija kuhusu masuala ya Uraia na Utawala Bora.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo mapema leo Machi 03, 2025 wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya Wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa kuhusu Elimu ya Uraia na Utawala Bora ambapo yamewakutanisha Kamati ya Usalama ya Mkoa, Kamati za Usalama za Wilaya, baadhi ya Wataalam wa Halmashauri na Watendaji wa Kata zote za Mkoa wa Mwanza.
“Ninafahamu kuwa wote tunaoshiriki mafunzo haya tunawawakilisha viongozi walio chini yetu na ni imani yangu kuwa mafunzo haya yatatusaidia kuongoza kwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora”.