Atukuzwaye
Senior Member
- Oct 5, 2026
- 191
- 250
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (RC), Said Mtanda ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kuwakamata ndani ya saa 24 wote waliohusika na wizi wa betri 40 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, huku akiwataka walioziiba kuzirejesha mara moja. Mtanda alitoa agizo hilo jana jioni Jumatatu, Oktoba 19, 2026, wakati wa ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, baada ya kupata taarifa za wizi wa betri hizo pamoja na kifaa cha kubadilisha chanzo cha umeme (changeover switch).
Amesema anashangazwa na namna betri hizo zilivyoweza kuondolewa hospitalini hapo bila watu wanaosimamia mali hizo kugundua mapema, akitaka uchunguzi ubaini waliohusika na jinsi walivyofanikiwa kuzitoa. “Betri 40 zinawezekanaje kuondoka hospitali kama hii watu wasiwe wanajua? Zilikuwa zinahifadhiwa wapi,” amehoji Mtanda.
Amehoji pia ufanisi wa ulinzi na usimamizi wa mali za hospitali hiyo, akisema uwepo wa milango na walinzi unapaswa kusaidia kulinda vifaa vya Serikali. “Hapa zimehifadhiwa ndani, kuna milango inafunga na kuna watu, kuna walinzi hapa,” amesema. Mtanda amesisitiza Serikali haitavumilia wizi wa mali za umma, akitaja pia matukio ya wizi wa magodoro, dawa na vifaa vingine yaliyowahi kuripotiwa hospitalini hapo.