Wana jamvi, kuna Mkuu wa mkoa mmoja Anaitwa Saidi Mohamed Mtanda ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyepokea Kijiti kutoka Kwa Amos Makala akitokea Mkoa wa Mara baada ya kuwa Mkuu wa wilaya kwenye wilaya kadhaa hapa nchini.
Mwanza ndiyo Mkoa wake wa Kwanza kuongoza tangu ateuliwe kukaa kwenye kiti hicho kikubwa kabisa kwa ngazi ya mkoa, Mwanza ni mkoa wenye idadi Kubwa ya watu ukilinganisha na Maeneo yote aliyopita kama Kiongozi wa Umma.
Wakati anakabidhiwa ofisi takribani miezi 7 iliyopita kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkoa Pamoja na mambo mengine aliahidi kutimiza majukumu yake Kwa mujibu wa katiba,sheria na miongozo iliyopo.
Lakini katika kipindi ambacho hata Mwaka Mmoja hajatimiza kama Mkuu wa Mkoa huo tunashuhudia akiingia kwenye kashfa kadhaa ambazo zinamtia doa Mteule wa Mh Rais Samia Suluhu Hassan .
Aibu ya Kwanza na iliyowashtua wengi ni pale alipotajwa kwenye sakata la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Yahya Nawanda anayeshtakiwa Kwa madai ya kumlawiti mwanafunzi wa chuo Kikuu kimoja jijini Mwanza.
Katika taarifa ya mlalamikaji aliyejulikana kama Tumsiime Ngemela , Mh RC SAID MTANDA alitajwa kuinjinia katika kuizima kesi Ili sifike mahakamani kwa kumshawishi huyo Binti akubali kupokea pesa Ili kumlinda mtuhumiwa bwana Nawanda.
Hapa RC Mtanda aliwashangaza wengi na kujiuliza kuhusu kile kiapo chake cha kuilinda katiba ya Tanzania,watu walijiuliza kama anawatoto lakini wapo walioenda mbali zaidi kuwa huenda nayeye ni mshiriki hadi kuliona suala Hilo ni dogo na halipaswi kufikishwa kwenye vyombo vya Dola.
Anyway tuachane na Hilo maana huyu bwana kalalamikiwa pengi wakiwepo waandamizi na mashabiki wa Soka, ndiyooo.....
amelalamikiwa na baadhi ya viongozi wa Jiji na wilaya ya Nyamagana Kwa kuhodhi madaraka wakati wa kuisaidia Pamba Jiji FC kupanda daraja na hata baada ya kupanda daraja alidaiwa kushinikiza kusajiliwa Kwa baadhi ya wachezaji huku akiwasikiliza watu wa nje zaidi kuliko wamiliki wa timu.
Inasemekana Mtanda aliwakazimisha viongozi wa Jiji kuwalipa baadhi ya marafiki zake aliowaita kutoka Dsm Ili waje kumshauri kuhusu namna ya kulifanya tamasha ya Pamba Jiji FC wengine wakilala kwenye hoteli ya Nyota Tano Kwa gharama za Jiji,Hivi kweli Jiji hakuna watu wakuratibu shughuli kama Ile?
Huyo bwana Mkubwa inadaiwa ndiye aliyehusika kuwaondoa baadhi ya viongozi waliosaidia Timu Kwa muda mrefu bila kujali nguvu walizotumia katika kuijenga Timu lakini pia ndiye aliyeshinikiza kuondolewa Kwa wadhamini wakuu Jambo food ambaye aliisaidia Timu wakati ikiwa na hali mbaya na kusahau Wema wote alioifanyia klabu.
Na inaelezwa kuwa kwa maslahi binafsi alishinikiza kuvunjwa Kwa gharama kubwa Kwa mkataba wa Pamba Jiji FC na kampuni ya vifaa vya Michezo ya Netsports na kushinikiza udhamini wa GSM.
Hatua hii imetafsirisa kama sehemu ya kuinasibisha Pamba Jiji FC na Yanga kwakua yeye ni mwanachama wa Yanga na komandoo mstaafu wa Yanga kabla ya kushika wadhifa alionao .
Kwa mujibu wa watu wake wa karibu wanadai kwamba RC Mtanda hashauriki imefika wakati hata wasaidizi wake wameamua kumuacha afanye analotaka.
Mipango yake ya kuinasibisha Pamba Jiji na Yanga ndiyo iliyochochea kile kilichotokea mwishoni mwa juma kama ambayo Imeshuhudiwa na vyombo vya habari na baadaye taarifa Rasmi ya Simba akidaiwa kusababisha taflani kuelekea mchezo wa Pamba Jiji FC dhidi ya Simba SC pale ambapo aliamua kutinga uwanjani na askari polisi Ili kuwanusuru vijana wake wa Pamba na Yanga waliokuwa wamejibanza uwanjani wakitega mabomu yao na Mganga wa jadi kabla ya kushtukiwa na makomandoo wa Simba.
Inasemekana vijana hao waliposhtukiwa walimpigia simu bosi wao RC Mtanda Ili aje awanusuru lakini Kwa bahati mbaya na vile hataki Ushauri Kiongozi huyo akaona aende front mwenyewe kuhakikisha anaiharibia Simba Kwa namna yoyote ile lakini Kwa bahati mbaya mipango yake na wenzake ikagonga Mwamba.
Kifupi hakukuwa na Sababu ya yeye kwenda uwanjani wakati Kuna vyombo vya Dola kama kulikuwa na tishio la usalama ni dhahiri yeye asingeweza kutuliza bila nguvu ya Polisi kumbe Kwa yeye kwenda na kama alivyosema alienda kwasababu alihofia askari peke yao kutekeleza wajibu wao bila weledi, Kwa kauli hiyo ni wazi ipo haja kwa yeye kuliomba radhi Jeshi la Polisi maana ni kama analishushia hadhi kwamba Kuna wakati linatekeleza majukumu yake bila weledi hadi wasimamiwe na wakuu wa mikoa hii ni aibu.
Tumeona kuna baadhi ya wakazi wa Mwanza na wanasiasa wameanza kumsema kuwa amewadhalilisha Sasa huu ni wakati wa Mamlaka za Uteuzi zimuangalie vyema kabla hajaendelea kuwadharirisha.
MWANZA ni Mkoa wenye changamoto nyingi acha za Wananchi wanadhurumiana ardhi,wafanyabiashara wanalia na miundombinu,wanafunzi hawana madawati,uvuvi haramu wakulima nao wanazo changamoto zao,lakini huduma za maji na umeme nazo zimekuwa kikwazo cha maendeleo ,Kwa hiyo huu ni wakati wa Viongozi akiwepo huyo Mkuu wa Mkoa SAID MOHAMED MTANDA kujikita kwenye kushughulikia mambo ya msingi kuliko kukalia ushabiki wa Simba na Yanga ambao haunafaida na maendeleo yetu hapa Mwanza..
Kwenu wanajamvi…
Shaloom