Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mambo hayo, kwani matokeo si huwa yanajionesha tu? Kitu kikijitembeza ndio unatuambia hamna kitu hapo, ni garasa.
====
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala leo Novemba 18,2024 anafanya ziara katika bandari ya Mtwara akiwa na Vyama 15 vya siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa lengo la ziara hiyo ya kuambatana na Vyama vya siasa ni kujionea hali halisi inayoendelea katika bandari ya Mtwara ili wakawambie wanachama wao namna serikali ilivyowekeza katika bandari na shughuli zinazofanywa kwani Mtwara ni kitovu cha uchumi katika eneo la kusini mwa Tanzania.
Aidha amesema kuwa kutokana na serikali kuwekeza zaidi ya bilioni 157.8 na kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kusafirisha korosho zote, simenti, makaa ya mawe na vitu vingine, na shughuli zote wazione vyama vya siasa ili wajenge Mtwara kwa pamoja.
Kwa upande katibu wa CUF Mtwara mjini Ndg. Saidi Kulugha kwa niaba ya Vyama vyote vilivyotembelea Bandarini hapo amesema kuwa wameshukuru kwa kuwathamini vyama vya siasa kujionea wenyewe Mambo yanayofanywa na serikali kwani wamepita wakuu wengi hawakuwahi kufanya hivyo apo awali kwani wanaamini wataendelea kushirikishwa katika mambo mengine.
Vile vile amesema jambo ili lisiwe wakati huu kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, maana watu wanaweza kutafasiri tofauti kuwa labda sehemu ya kampeni wakati ni utaratibu wa kawaida tu.
Hata hivyo Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand Nyathi amesema kuwa hadi sasa wamehudumia meli 5 zilizofungasha makasha na wamehudumia takribani tani elfu 79, huku wanaendelea kuhudumia meli zingine, pia amesema amefurahishwa kutembelewa na vya vya siasa bandarini hapo ili kujionea kazi zinazofanywa.
Safari Media