RC Mwanamvua Mrindoko azindua basi la Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi

RC Mwanamvua Mrindoko azindua basi la Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
RC MRINDOKO AZINDUA BASI LA WATUMISHIKATAVI RRH, ATOA PONGEZI KWA UTOAJIHUDUMA BORA KWA WANANC...jpg

RC MRINDOKO AZINDUA BASI LA WATUMISHIKATAVI RRH, ATOA PONGEZI KWA UTOAJIHUDUMA BORA KWA WANANC...jpg
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, Mei 20, 2026 amezindua rasmi Basi la Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi.

Akizungumza mbele ya Watumishi, Mrindoko amesema Basi hilo litasaidia sana Watumishi kupunguza gharama za maisha kwa kuwarahisishia usafiri.

Pia soma ~ Milioni 100+ zinatumika kununua gari la ‘staff’ Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi wakati hospitali haina mochwari

Kwa upande mwingine, Mrindoko amewapongeza Watumishi wote wa Katavi RRH kwa kazi nzuri ya kutoa Huduma bora ya Kuwahudumia Wananchi.
RC MRINDOKO AZINDUA BASI LA WATUMISHIKATAVI RRH, ATOA PONGEZI KWA UTOAJIHUDUMA BORA KWA WANANC...jpg
RC MRINDOKO AZINDUA BASI LA WATUMISHIKATAVI RRH, ATOA PONGEZI KWA UTOAJIHUDUMA BORA KWA WANANC...jpg
"Mimi tangu hii Hospitali ianzishwe hapa Katavi sijawahi kutoka nje ya Mkoa kwenda kutibiwa, Huwa nakuja hapa kupata matibabu kwasababu huduma ni nzuri na kuna kila aina ya matibabu hapa. Niwapongeze sana KRRH," amesema Mrindoko.

Naye, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dr. Deogratias Banuba amesema wazo la kununua Basi hilo Dogo aina ya TATA alilipata tangu mwaka jana 2025 na lengo lilikuwa kuwarahisishia usafiri Watumishi ili kuwahi kazini na pia kutumiwa kwenye matukio ya kijamii.

Pia soma ~ Madai ya kukosekana Mochwari Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, uongozi wasema fedha imetengwa kujenga jengo hilo
 
Wajengewe hostel wakae jirani na hospital.
 
Back
Top Bottom