Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,653
- 31,010
Sasa hivi wanasiasa wanashindana kujenga nyumba za umma kwa hela kiduchu ili kumridhisha aliyewateua.
Tena wanafanya hivyo mbele ya kamera ili waonekane kama huyu RC.
Tunaomba wakitoa maagizo ya kupunguza gharama za ujenzi, waweke maagizo hayo kwa maandishi yenye sahihi ili kuonyesha uwajibikaji wao pindipo jengo litakapo anguka kwa kukosa viwango.
Watu wanajidai kujua fani hii ya ujenzi, twaomba vile vile wasiishie kutoa maagizo-waweke sahihi ya hizo variations in cost.
Jengo la umma litakapo anguka na kuua muwajibikaji(RC) naye achukuliwe hatua.