RC Mwanza, Mtanda alivyosema Yanga Oyee! Akiwahakikishia wadau Ushindi kwa Pamba Jiji dhidi ya Simba SC mechi yao ya Ligi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda alipokuwa anaongelea maandalizi ya Pamba Jiji kuelekea mechi ya kuikabili Simba SC, kesho Novemba 22, akiwahakikishia wasikilizaji kuwa katika game hiyo ushindi ni lazima wa Klabu hiyo ya Rock City, katika Uwanja wa Ccm Kirumba.

Amesema hayo akiwa Kwimba kwenye shughuli za Kiserikali mbele ya viongozi mbalimbali wa Wilaya hiyo.

"Pamba jiji kesho kutwa (Ijumaa) tunajua tunacheza na Simba, matarajio yetu ni kuwafunga Simba, Sasa wengine hawaamini ila mimi nawaambia kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu Simba inaenda kufungwa na Pamba, lakini kama hawaamini waende wakaangalie namna ambavyo Yanga alifungwa na Tabora..." (Yanga Oyee!)
 
Kitu kidogo kwenye mpira kinaweza kuja kumuathiri kwenye siasa.
Yeye anaongoza wapenzi wa timu zote. Ameamuwa kuwagawa. Ipo siku.
Wapi ameonesha kuwagawa yeye anatamba na Team ya Mkoa wake kakosea wapi??
 
Attachments

  • IMG-20241121-WA0075.jpg
    IMG-20241121-WA0075.jpg
    73.2 KB · Views: 4
Watu wengi wasichokijua mashabiki wa Pamba ni mashabiki wa Simba.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda alipokuwa anaongelea maandalizi ya Pamba Jiji kuelekea mechi ya kuikabili Simba SC, kesho Novemba 22, akiwahakikishia wasikilizaji kuwa katika game hiyo ushindi ni lazima wa Klabu hiyo ya Rock City, katika Uwanja wa Ccm Kirumba.

Amesema hayo akiwa Kwimba kwenye shughuli za Kiserikali mbele ya viongozi mbalimbali wa Wilaya hiyo.

"Pamba jiji kesho kutwa (Ijumaa) tunajua tunacheza na Simba, matarajio yetu ni kuwafunga Simba, Sasa wengine hawaamini ila mimi nawaambia kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu Simba inaenda kufungwa na Pamba, lakini kama hawaamini waende wakaangalie namna ambavyo Yanga alifungwa na Tabora..." (Yanga Oyee!)
View attachment 3158258
Hela ya GSM imemtoa akili huyu mmakonde
 
Back
Top Bottom