sifi leo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2012
- 5,182
- 8,948
Habari ya asubuhi wadau?
Ninaomba nitoe rai kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kutokana na hali halisi niliyoiona tangu nimeingia mkoa wa Mwanza wiki iliyopita.
Kwanza kuna mikusanyiko mingi sana kwenye baa Mwanza Mjini kuanzia saa moja jioni na kuendelea.
Pili kuna wafanyabishara wengi na wananchi wengi hawajachukua hatua yoyote mfano leo nmetembelea maeneo ya Dampo na kwenye masoko mengine yani watu wako bize na biashara hakuna hatua yoyote ya kujinga na maambukizi iliyochukuliwa.
Hakuna ndoo za maji za kuosha mikono kwa wajasiriamali.
Wafanya biashara zaidi ya 150 hakuna aliyevaa barakoa hata mmoja na akipita aliyevaa barakoa anazomewa au kuonekana ni mgonjwa tayari.
Pongezi ni kuwa ni Rock City Mall tu ndio huruhusiwi kuingia na kutoka pasipo kuvaa barakoa.
Cha ajabu na cha kushangaza ambacho kimenisukuma nije na bandiko pale mlangoni kuna vijana wanauza barakoa shilingi 1000 ama huna basi wanakukodisha kwa shilingi 500 unavaa uningia ukitoka unawarudishia wanakodisha wengine na wateja wao wakubwa ni bodaboda ambao wanatozwa 200 tu.
Wito wana habari nchini msisubiri majibu ya wamekufa wangapi wamepona wangapi ingieni mtaani mwelezee umma wa watanzania kinachotakiwa kufanyika.
Nipo Mwanza kwa sasa ntasema kweli daima kuwalinda wananchi wenzangu.
Sent using Jamii Forums mobile app