John John Msakuzi
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 296
- 103
::
MKuu huyo wa Mkoa wa Tabora mbele ya Waandishi wa habari amesema Rais Samia ameongeza Mapato ya Madini Tabora kutoka TZS 40bn hadi TZS 133bn ndani ya miaka minne(4).
Katika kipindi cha 2021 hadi 2025, Serikali chini ya Rais Samia imeimarisha sekta ya madini mkoani Tabora kwa kuongeza uzalishaji wa madini kutoka tani 0.34 mwaka 2020 hadi tani 0.8 mwaka 2025,
Thamani ya fedha za kigeni zilizopatikana kutokana na uuzaji wa madini ikiongezeka kutoka USD15,068,988 au TZS 39.5 bilioni mwaka 2020 hadi USD60,692,090.41 sawa TZS 133.0 bilioni mwaka 2025.
Mapato ya Halmashauri kutoka sekta hiyo yameongezeka kutoka TZS118.63milioni mwaka 2020 hadi TZS399.06milioni mwaka 2025. Aidha, vituo vya madini vimeongezeka kutoka kituo 1 mwaka 2020 hadi vituo 5 mwaka 2025, na leseni za wachimbaji wadogo kutoka 136 mwaka 2020 hadi 574 mwaka 2025