Pre GE2025 RC Ruvuma: Dkt. Ndumbaro hana deni jimbo la Songea mjini utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Pre GE2025 RC Ruvuma: Dkt. Ndumbaro hana deni jimbo la Songea mjini utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas,amemsifu Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Dk Damas Ndumbaro kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo katika jimbo hilo.

Kanali Abbas ametoa kauli hiyo mbele ya wananchi wa Kata ya Subira, Manispaa ya Songea, wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi wa uchimbaji wa visima vya umwagiliaji kwa mkandarasi kutoka Kampuni ya MNFM Construction Co.

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amesema kuwa tangu alipofika mkoani Ruvuma, Dk Ndumbaro alimueleza kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa jimboni humo na kuahidi kufuatilia utekelezaji wake.

"Niliandika vipaumbele tisa alivyonieleza, vinavyohusiana na barabara, afya, elimu, kilimo na michezo, Kila nilipotembelea mradi, nimekuwa nikiweka alama ya vema kwa yale yaliyotekelezwa, hadi jana nilikuwa nimekamilisha mambo nane, na leo hapa Subira naweka tiki ya tisa. Kwangu mimi, hana deni," amesema Kanali Abbas.

Katika awamu ya kwanza ya mradi huu wa uchimbaji wa visima, kazi itaanza katika Kata ya Subira, Mtaa wa Kihekwa, ambapo zaidi ya wananchi 100 watanufaika.
Visima hivyo vitasaidia wakulima wa mazao mbalimbali kama mahindi, viazi vitamu, mboga mboga na maharage, hivyo kuongeza tija katika kilimo cha umwagiliaji.

Chanzo: Habari Leo
 
Back
Top Bottom