Raphael Alloyce
Senior Member
- Nov 15, 2020
- 128
- 372
Hii kesi ya Ulawiti dhidi ya huyo binti (Mwanafunzi) inabidi kuchunguzwa kwa makini sana. Bado kuna maelezo mengi sana hata kwa binti mwenyewe.Hapa nasikiliza video ya Binti Tumsiime anayedaiwa kulawitiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Nawanda. Binti ameelezea kwa kina sakata zima la kulawitiwa, mpaka msukumo mzima wa kutaka kuzima kesi.
Binti Tumsiime ameelezea kuwa baada ya kufanyiwa kitendo kile, aliripoti kituo cha polisi kwa hatua za kisheria zaidi. Wakati akiwa na Polisi wakifanya uchunguzi na kukusanya ushahidi, ghafla alitafutwa na RC Mtanda ambaye alitaka waonane ofisini kwake, binti anadai alikataa na kusema yupo na polisi lakini RC Mtanda alitumia mamlaka yake na hatimaye kuonana na binti huyo.
Binti anadai baada ya kufika Ofisini kwa Mtanda, RC huyo alimsihi suala hilo aliondoe polisi ili limalizwe kifamilia ila binti aliamua kukaza. Anadai kuwa akiwa ofisini RC Mtanda aliongea kilugha na Dkt. Nawanda (nadhani kimakonde).
RC Mtanda aliwaita Polisi waliokuja na binti huyo na kuwaambia ameshaongea na Binti na kesho wampokee vizuri anakuja kufuta kesi. Binti hakufanya hivyo kama alivyotakiwa kufanya na RC Mtanda.
Kwa mujibu wa binti huyo, RC Mtanda aliendelea kuinjinia mpango mzima wa kuzima sakata ikiwa ni pamoja na kushiriki kumwandikisha barua feki ya kufuta kesi, kumshawishi mama mzazi wa binti nk nk.
Hoja yangu hapa; RC Mtanda kama kiongozi wa umma alipaswa kuwa mstari wa mbele kuheshimu na kusimamia sheria, badala yake anatumia mamlaka ambayo tumempatia kutaka kudhulumu haki ya Tumsiime.
Rais Samia, Watanzania hatutakuelewa endapo RC Mtanda ataendelea kuwa Mkuu wa mkoa, amekosa sifa za kuwa mfano wa kuigwa.
Aione mama yetu Dkt. Gwajima D
Pia soma
Kuanzia kukutana na RC, RC kumtaka kimapenzi na yeye kukubali ilihali anatambua bado ni Mwanafunzi na kisha kwenda na RC maeneo ya faragha kwa kusudi ya kuvunja amri ya sita.
Na alivyoingiwa kinyume na maumbile, kiukweli bado kuna maswali mengi sana... Hapa inabidi uchunguzi/upelelezi wa kina kufanyika na sio kutumia hisia. Kamwe tusiruhusu hisia kutuongoza.