#COVID19 RC Sengati: Kiongozi wa CHADEMA aliyesema Shinyanga imeelemewa na wagonjwa wa corona achukuliwe hatua kali za kisheria

Na aliyesema bosi anachapakazi,
Aende wapi sokoni kariakoo,tandale
Alifanywaje?
 
Kiongozi wa chadema alisema uongo kuwa kuna wagonjwa wengi.
Ukweli ni kuwa kuna wagonjwa wangapi?
(0, 1, 2, 3, 4, ..........)
Bila maelezo yenye namba, upuuzi ni ule ule.
 
Huyo RC anatafuta adhabu iliyotembea tarehe 17/3/2021
 
Kwa mara ya kwanza kuona kiongozi kwenye ngazi ya serikali duniani akitembelea wodi ya wagonjwa wa Covid inayopaswa kuwa ni sehemu ya karantini...
 
Amekuta wagonjwa wangapi wa corona kwenye hospital aliyokwenda?

Kwenye vituo walivyovitaja, kuna wagonjwa wangapi kwa kila kituo?

Kwenye kila kituo wagonjwa wote wana mitungi ya gesi ya kuwasaidia katika matibabu?

Kwa wagonjwa waliopo, kuna ziada au upungufu wa mitungi ya gesi mingapi?

Rc njoo na takwimu (idadi) ya wagonjwa ili tumhukumu kiongozi wa bavicha.

Mkoani Shinyanga mbio za mwenge zinaendelea,

Je, tahadhali zinachukuliwa katika maeneo yote mwenge unapopita na kulala?

Kama kuna wagonjwa wa Corona mkoani Shinyanga, kwa nini mbio za mwenge zisiahirishwe ili KUWAKINGA Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga?

Rc watendee HAKI Wananchi wa Shinyanga.
 
Mbona sasa watu wanaombwa hela wapendwa wao wawekewe oxygen sababu mitungi ni michache au hajui hilo?
 
Huyo RC mpumbavu sana badala ya kutumia muda huo kuonyesha kipi ni ukweli na kipi ni uongo yeye anawahi kwenye vyombo vya dola. Sasa hapo wagonjwa wengi wanaanzia wangapi?Kuelemewa kwa tafsiri yake ni kufanyaje?Jinga kabisa Hilo bado lipo enzi ya utawala mwendawazimu
 
Du anapata wapi guts za kusogelea wagonjwa wa corona hatari sana
This tells it all kuwa Kuna wagonjwa , Sasa anajifanya kwenda huko kuonesha kuwa hakuna wagonjwa wengi.
 
Kiongozi wa chadema alisema uongo kuwa kuna wagonjwa wengi.
Ukweli ni kuwa kuna wagonjwa wangapi?
(0, 1, 2, 3, 4, ..........)
Bila maelezo yenye namba, upuuzi ni ule ule.
Nashindwa kuelewa huko Shinyanga wengi ni wangapi? Wana shule nzuri inayofundisha hisabati pale Mjini kati Shycom wawasaidie kufafanua "wengi' ni wangapi? Au shinyanga ina tafsiri tofauti?
 
Kanda ya ziwa kuna tatizo... Moja aliwahi kusema..ni ka-mafua...imekoromea mbali...kilichotokea imebaki historia. Kosa la huyo kiongozi wa Bavicha slioni.. Ni tahadhari
 
Hakuna haja ya kupaniki. tatizo la ugonjwa huu lipo na tuendelee kuchukua tahadhari. Kauli zingine ni za kutuamsha tu usingizini na siyo kutolea tamko kila kauli za wadau. Tuendelee kuelimishana badala ya kutishana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…