The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha ameweka jiwe la msingi Shule mpya ya sekondari Bumva, Kijiji cha Bumva Kata ya Segese Halmshauri ya Wilaya ya Msalala iliyojengwa kwa gharama ya Sh. Milioni 603,890,563/=.
Shule hiyo inatarajiwa kupokea wanafunzi zaidi ya 100 kutoka shule za sekondari ya Mwalimu Nyerere na Segese wanaotoka katika vijiji vya Bumva, Busongo C, Wisolele na Senta Mashariki kwa vitongoji vya Misungwi na Itembe.
RC Macha amesema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha na kusogeza miundombinu ya elimu kwa wananchi ili kuhakikisha watoto wenye umri wa kwenda shule wanapata elimu na sio kuwatumikisha mashambani na kuchunga mifugo.
Amesisitiza miundombinu hiyo iendelee kutunzwa na kuzingatia suala la utunzwaji wa mazingira ikiwemo upandaji wa miti.
Katibu Tawala wa Mkoa CP Salum Hamduni amesema Serikali inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali. Zaidi ya Bilioni 6 ndani ya Mkoa wa Shinyanga zimetolewa ambayo inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya Bumva inayoendelea kujengwa kwa kiasi cha Sh. Milioni 603,890,563/= na hivyo kuweza kusogeza huduma ya upatikanaji wa elimu karibu na wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Rose Manumba amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri hiyo ikiwemo shule ya Sekondari Bumva ambayo inakwenda kupunguza adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu na utoro sugu.
Aidha DED Manumba amewataka Watumushi wa Halmashauri hiyo kuendeleza jitihada na kasi ya usimamizi na utekelezaji wa miradi mingine inayoendelea kutekelezwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati kwa kuzingatia ubora wa mradi na thamani ya pesa ionekane.