RC Simiyu aagiza Afisa Kilimo wa Wilaya Meatu ahamishwe kwa kushindwa kutekeleza majukumu kikamilifu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi amemuagiza katibu Tawala Mkoa wa Simiyu kumhamisha mara moja kituo cha Kazi Afisa Kilimo wa Wilaya ya Meatu, Thomas Shilabu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Aidha, Kihongosi amemuagiza katibu Tawala Mkoani Simiyu kuwabadilishia vituo vya kazi wakuu wa Idara na Sehemu wote ambao wamekaa muda mrefu katika vituo vyao vya kazi ili kuimarisha utendaji kazi ndani ya Mkoa wa Simiyu.

Hatua hiyo inajiri baada ya baadhi ya Wakazi wa Kijiji cha Mwabusalu kutokuwa na taarifa kuhusu uwepo wa ruzuku katika mbegu za mahindi wakiiomba serikali kuwapatia mbegu hizo kwa ruzuku.

Kihongosi yuko katika ziara ya siku 3 Wilayani Meatu kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi.

GCO,
Simiyu RS
12 Novemba 2024.

 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-11-12 at 12.52.26_bcb63d7d.jpg
    136 KB · Views: 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…