Pre GE2025 RC Simiyu afanya matembezi ya kumuombea Rais Samia na Taifa. Chawa kazini kujihakikishia nafasi!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Harakati za kujikomba na kulamba miguu zinazidi kupamba moto. Kenani Kihongosi ameongoza kupe wenzake kumuombea Rais Samia, taifa liwe na baraka tele.


Ni mwendo wa kujiweka karibu na Rais na kusikika kadri iwezekanavyo ili usisahaulike kwenye ufalme wa bwana, teh teh ufalme wa mama😂😂.


Hawakosi watu bana, mmoja akitaangaza jambo wote inabidi wajitokeze, ubaki nyuma halafu uingizwe kwenye kitabu cheusi, subutuu!


Yangefanyika matembezi haya haya kuombew waliopotezwa na wasiyojulikana, ungesikia ni chonchezi, polisi wangefanya matembezi hayo badala yake.


Watanzania bado tunakoroma.😴😴
 
Ni moja kati ya wanasiasa bora sana nchi hii kuwapata baada ya Majaliwa na Dotto Biteko chini ya uongozi wa SSH
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…