Rc Simiyu,Kenan Kihongosi akemea majungu,fitina na chuki kwa wafanyakazi

Rc Simiyu,Kenan Kihongosi akemea majungu,fitina na chuki kwa wafanyakazi

Mwanantogakulya

Senior Member
Joined
Mar 18, 2025
Posts
157
Reaction score
155
MKUU wa mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi, amewataka watumishi wa umma mkoani humo kuachana na tabia za fitina, majungu na chuki katika maeneo ya kazi, akisisitiza kuwa hali hiyo inachangia kuporomoka kwa tija na kuathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akizungumza Mei Mosi,2025, wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Nguzonane wilaya ya Maswa, amesema vitendo hivyo vimekuwa vikiwanyima watumishi morali ya kazi na kuvuruga mshikamano unaohitajika ili kufanikisha malengo ya serikali.

Amesema kuwa katika baadhi ya halmashauri na idara za serikali,hali hii imewahi kusababisha hata kusambaratika kwa timu za usimamizi au kushindwa kutekelezwa kwa miradi ya maendeleo kutokana na
kutokuwepo kwa mshikamano.

"Tujenge upendo na mshikamano miongoni mwetu. majungu, chuki na fitina vinaua morali ya kazi na vinarudisha nyuma jitihada za maendeleo,serikali inahitaji watu wanaofanya kazi kwa moyo mmoja," amesema.

Aliongeza kuwa,watumishi wanaoweka mbele maslahi binafsi kwa kutumia njia za kudhalilisha wenzao hawawezi kujenga taasisi imara, bali huchangia migogoro isiyo ya lazima kazini.

Pia amewataka viongozi wanaoongoza taasisi za serikali kuhakikisha wanazitumia vizuri kwa kutoa huduma kwa wananchi sambamba na kuwasimamia walio chini yao kwa kufuata taratibu zilizowekwa na siyo kuwanyanyasa.

IMG_8846.JPG
 
Back
Top Bottom