GE2025 RC Sirro: Diamond alisema sahihi, msilalamike fanyeni kazi

GE2025 RC Sirro: Diamond alisema sahihi, msilalamike fanyeni kazi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro, amewataka vijana kutumia muda wao kufanya kazi kwa bidii badala ya kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kulalamika.

Sirro amesema vijana wanapaswa kujiuliza kila siku, kuanzia asubuhi hadi jioni, ni kazi gani wamefanya kwa ajili ya familia na taifa lao.

“Niliona Diamond Platnumz walimkosoa, lakini alichosema ni sahihi. Nikiwa Balozi nchini Zimbabwe niliona watu wanafanya kazi kwa bidii. Ukiwaambia wafanye kazi bustanini, watafanya kuanzia saa moja asubuhi hadi saa kumi jioni mpaka uwaambie wapumzike. Lakini sisi, ukimpa mtu kibarua, dakika chache tu unamwona amesepa. Sasa maendeleo hayawezi kuja kwa kusepa. Utasepa mpaka lini?” amehoji RC Sirro.

Hivi karibuni, msanii wa muziki Nassib Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, alikosolewa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii baada ya kusambaa video yake akiwaasa vijana kufanya kazi badala ya kulalamika. Katika video hiyo, Mondi anasisitiza kwamba mafanikio yake yametokana na kazi, si malalamiko.

Sirro ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano maalumu na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kuhusu hali ya ulinzi na usalama mkoani Kigoma, hususan katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025.

 
Vp khs tusi la diamond, Mkuu wa mkoa amesemaje? au hicho kipande hajakiona 😂
 
Amekuwa msemaji wa mondi.yeye mwenyewe mvivu namba moja.amestaafu bdo anapewa cheo kngne ndyo amestaafu au? km yeye ni mwanaume aje tutafute wote cyo kubebw kwa hisani ya chama km fadhila ya kukandamiza chadema kwa intelejisia feki
 
Kwani watanzania hawafanyi kazi?
Kwani serikali inajukumu la kuwalisha watanzania?

Mimi nadhani wanachopigia kelele watanzania ni usawa na haki.

Yaani wanachokifanya kiwe sawa na wanachokipata. Na wenye jukumu la kutengeneza mazingira ya usawa ni waliopewa dhamana ya kutuongoza
 
Kweli nimeamini ukiingia tu si si emu, na akili yote inahama kutoka kichwani, na kukimbilia tumboni.
NB:- Hiki nilichokiandika hapa, hakina uhusiano na mada inayojadiliwa.
 
Back
Top Bottom