GE2025 RC Sirro: Hatukatazi watu kukaa vikundi lakini mnakaa kwa lengo gani?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro amesema kuwa hawakatazi watu kukaa vikundi wakati ama baada ya kupiga kura kesho Oktoba 29 2025, kama watu hao watakuwa wanajadili mambo ya kawaida tu.

Balozi Sirro amesema itakuwa shida tu pale watu hao wanaokaa vikundi wakiwa na lengo la kutaka kuvuruga shughuli za uchaguzi ndipo vyombo vya usalama vitaweza kuwachukulia hatua.

"Hatukatazi watu kukaa vikundi, lakini mnakaa vikundi kwa lengo gani. Kama mnakaa vikundi kwa lengo la usalama kuzungumza maendeleo ya nchi yetu na mambo ya uchaguzi bila fujo, sisi hatuna shida. Shida yetu ni kudili na wale wanaotaka kufanya fujo na wale ambao wanataka kuzuia watu wengine kutimiza haki yao ya kufanya uchaguzi, wale ndio adui wa kwetu na vyombo vya usalama," amesema Balozi Sirro.

Alikuwa akizungumza leo Oktoba 28, 2025 kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1, akizungumzia hali ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu kesho Oktoba 29, 2025.
 
Huyu naye ni hasara tu kwa Taifa. Wenzake baada ya kustaafu wamepewa uenyekiti wa bodi ya mashirika na taasisi zenye ulaji! Yeye amepewa Ukuu wa Mkoa, na amekubali eti! Ingengekuwa ndiyo mimi, ningekataa.
Ndugu yangu, hapo nikupinge kidogo. Mwenyekiti ni mtu wa kuchair vikao na kulipwa posho tu. Mara nyingi vikao ni vinne kwa mwaka. Mkuu wa Mkoa ni ajira ya kulipwa kila mwezi.
 
Kama umemuelewa ni kwamba, Wenye Hekima na Uzoefu katika kulitumikia taifa wana nafasi zao. Huko walipompeleka huyo siyo levels zake.
Kwa akili yako kwa level aliyoifikia huyo na kote alikipita ni mtu wa kutolea macho mshahara?
Sijui umri wako, lakini utajisikiaje shule FEZA au ilbouru wakikupatia sasa hivi nafasi ya kwenda kuanza form one kwenye shule zao?
 
Wewe hujanielewa. Mtu anayeongelewa hapa, aliwahi kuwa mkuu wa jeshi la polisi nchini, na akastaafu kwa mujibu wa sheria. Hakukuwa na sababu ya kumrejesha tena kwenye kazi ya kuajiriwa!
 
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro amesema kuwa hawakatazi watu kukaa vikundi wakati ama baada ya kupiga kura kesho Oktoba 29 2025, kama watu hao watakuwa wanajadili mambo ya kawaida tu.
Tunapangiana cha kujadili ? What's next hata kupangiana na mawazo ? Hii mbona kama inaingilia hadi uhuru binafsi ? Kama nalipa Kodi na kuwaweka waliopo Je ni kosa kwangu kujadili lolote na chochote kinachohusu Kodi yangu ?
 
Wewe hujanielewa. Mtu anayeongelewa hapa, aliwahi kuwa mkuu wa jeshi la polisi nchini, na akastaafu kwa mujibu wa sheria. Hakukuwa na sababu ya kumrejesha tena kwenye kazi ya kuajiriwa!
Ndugu yangu, kustaafu kusikie kwa jirani. Pamoja na kumjibu Consigliere alivyo niendea mazingira, ukistaafu inawezekana pesa isiwe tatizo ila kitu cha msingi ni matumizi ya muda kabla ya kulala. Kuwa na shughuli ya kufanya ni muhimu sana kwa mstaafu. Kwa maneno mengine afisi kwa wazanzibari au ofisi kwetu wabara. Ukuu wa mkoa kwa Sirro ni kumpatia ofisi ambapo akiamka asubuhi anaingia ofisini si kusoma magazeti au kuangalia TV na wajukuu. Nina uzoefu
 
Kama umemuelewa ni kwamba, Wenye Hekima na Uzoefu katika kulitumikia taifa wana nafasi zao. Huko walipompeleka huyo siyo levels zake.
Kwa akili yako kwa level aliyoifikia huyo na kote alikipita ni mtu wa kutolea macho mshahara?
Sijui umri wako, lakini utajisikiaje shule FEZA au ilbouru wakikupatia sasa hivi nafasi ya kwenda kuanza form one kwenye shule zao?
Kama utanilipia nakubali na nipo tayari kuwa nakuoshea vyombo mkuu Consigliere
 
Mkuu wa mkoa wa Kigoma anaenda kupigia kura viongozi wake walioko Dar es Salaam!
 
Ndugu yangu, kustaafu kusikie kwa jirani. Pamoja na kumjibu Consigliere alivyo niendea mazingira, ukistaafu inawezekana pesa isiwe tatizo ila kitu cha msingi ni matumizi ya muda kabla ya kulala. Kuwa na shughuli ya kufanya ni muhimu sana kwa mstaafu. Kwa maneno mengine afisi kwa wazanzibari au ofisi kwetu wabara. Ukuu wa mkoa kwa Sirro ni kumpatia ofisi ambapo akiamka asubuhi anaingia ofisini si kusoma magazeti au kuangalia TV na wajukuu. Nina uzoefu
Jambo la muhimu baada ya kustaafu ni kufanya tu mazoezi, kula chakula kisicho na athari kwenye afya yako, kupata muda mwingi wa kupumzika, kuwa karibu na familia, nk. Mtu ukifikia umri wa kustaafu, ni vizuri ukastaafu! Na siyo kurudishwa tena kazini, na wakati mtaani kuna vijana kibao tu wenye uwezo na hawana ajira.

Hivi vyeo vya kuteuana tena hata baada ya kustaafu, ni muendelezo tu wa kasoro ambazo wananchi tulizikataa kwenye Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ya Rais kupunguziwa mamlaka ya uteuzi na pia kuvifuta baadhi vyeo visivyo na tija kwenye karne hii ya 21; vikiwemo hivi vya Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
 
Naona matamko yamekuwa meengi

Kesho sio mbali ITAFAHAMIKA!
 
Ndugu yangu, hapo nikupinge kidogo. Mwenyekiti ni mtu wa kuchair vikao na kulipwa posho tu. Mara nyingi vikao ni vinne kwa mwaka. Mkuu wa Mkoa ni ajira ya kulipwa kila mwezi.
Sasa ukistaafu unahitaji ajira ya kulipwa kila mwezi ili iwaje? Umestaafu nini?
 
Huyu naye ni hasara tu kwa Taifa. Wenzake baada ya kustaafu wamepewa uenyekiti wa bodi ya mashirika na taasisi zenye ulaji! Yeye amepewa Ukuu wa Mkoa, na amekubali eti! Ingengekuwa ndiyo mimi, ningekataa.
Afanyaje alikuwa na option nyingine?
Maana hajipangii position
 
Jambo la muhimu baada ya kustaafu ni kufanya tu mazoezi, kula chakula kisicho na athari kwenye afya yako, kupata muda mwingi wa kupumzika, kuwa karibu na familia, nk. Mtu ukifikia umri wa kustaafu, ni vizuri ukastaafu! Na siyo kurudishwa tena kazini, na wakati mtaani kuna vijana kibao tu wenye uwezo na hawana ajira.

Hivi vyeo vya kuteuana tena hata baada ya kustaafu, ni muendelezo tu wa kasoro ambazo wananchi tulizikataa kwenye Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba ya Rais kupunguziwa mamlaka ya uteuzi na pia kuvifuta baadhi vyeo visivyo na tija kwenye karne hii ya 21; vikiwemo hivi vya Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Nakushukuru nimekusoma, umri ndilo tatizo.
 
Sasa ukistaafu unahitaji ajira ya kulipwa kila mwezi ili iwaje? Umestaafu nini?
Nakuelewa ni umri tu. Ukikua utanielewa zaidi au mtu aliye karibu Yako akistaafu ndipo utaelewa nasema nini. Ndugu zangu kustaafu kusikie kwa jirani
 
Back
Top Bottom