RC Telack Awakaribisha Wafanyabiashara Kushiriki Ufunguzi wa Gulio la Bidhaa za Usindikaji

RC Telack Awakaribisha Wafanyabiashara Kushiriki Ufunguzi wa Gulio la Bidhaa za Usindikaji

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

RC TELACK AWAKARIBISHA WAFANYABIASHARA KUSHIRIKI UFUNGUZI WA GULIO LA BIDHAA ZA USINDIKAJI.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack amewataka wafanyabiashara na wajasiliamali Mkoani Lindi kujitokeza kwa wingi kushiriki Ufunguzi wa Gulio la bidhaa za Usindikaji na Ushonaji linalotarajia kufanyika katika Viwanja vya Maonyesho ya Nanenane Ngongo, Manispaa ya Lindi ifikapo tarehe 02, Novemba mwaka huu.

Mhe. Telack ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza la Biashara Mkoa kilichofanyika Oktoba 17 ambapo kimewakutanisha wajumbe mbalimbali kutoka mashirika ya umma, sekta binafsi na wadau wa biashara Mkoani Lindi.

"Tarehe 2 Novemba tunakwenda kufungua minada au soko la kuuza bidhaa za usindikaji na ushoanji, wafanyabiashara na wajasiliamali tujitokeze kwa wingi kushiriki katika gulio hilo tuweze kujifunza kwa kujiongezea maarifa na ujuzi wa kuandaa, kuhifadhi bidhaa zetu na namna ya kupata masoko lakini oia tunatarajia kuwa na mawasilisho mbalimbali ambayo yataonyesha fursa zilizopo mkoani kwetu ambazo tunahitaji wafanyabiashara wa mkoa huu mzichangamkie hatutaki zikachukuliwe na watu wengine tuchangamke sisi kwanza. Na gulio hili tunatarajia kuwa linakwenda kuwa wa kwanza kufunguliwa nchini, twendeni na kwa pamoja tutatoka tukiwa na umoja" amesema Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Sekisheni ya Viwanda na Biashara Dkt. Bora Haule ameeleza kuwa kwa kuzingatia kuwa shughuli za uzalishaji wa bidhaa za usindikaji na ushonaji hufanywa na wanawake, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi imeandaa tuzo maalum kwa ajiri ya kuwatunuku wanawake vinara katika sekta hizo.

"Tuzo hizi zinasindikizwa na kauli mbiu isemayo 'ULIPO NDIPO WALIKUWEPO' lengo lake kuu ni kutambua mchango wa wanawake na umahiri wao katika kuhamasisha wengine kushiriki katika shughuli za usindikaji na ushonaji" ameongeza Dkt. Bora.

Uzinduzi wa Gulio la bidhaa za Usindikaji na Ushonaji linakwenda kutoa fursa ya wafanyabiashara na wajasiliamali kuuza bidhaa zao na kujitangaza huku mgeni rasmi katika tukio hilo akitarajiwa kuwa Mhe. Dkt. Seleman Jafo (Mb) Waziri wa Biashara na Viwanda.​

 

Attachments

  • Screenshot 2024-10-21 at 14-23-49 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-10-21 at 14-23-49 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    824.3 KB · Views: 1
  • Screenshot 2024-10-21 at 14-24-08 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-10-21 at 14-24-08 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    693.1 KB · Views: 1
  • Screenshot 2024-10-21 at 14-24-25 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-10-21 at 14-24-25 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    668.3 KB · Views: 1
  • Screenshot 2024-10-21 at 14-24-41 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-10-21 at 14-24-41 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    762.6 KB · Views: 2
  • Screenshot 2024-10-21 at 14-25-01 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-10-21 at 14-25-01 Mkoa Wa Lindi (@lindi_rs_) • Instagram photos and videos.png
    737 KB · Views: 1
Back
Top Bottom