RC wa Kagera, Chalamila asema Ng'ombe wanaofugwa kwa stress wana nyama ngumu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Untitled-1.png
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amewataka wadau wa mifugo kutoa elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji ili kuwawezesha kufanya ufugaji wa kisasa ambao utaepusha ng'ombe kutembea umbali mrefu kutafuta malisho na kusababisha nyama yake kuwa ngumu

Akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya wakulima - Nanenane - Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa ili kuhakikisha inapatikana nyama laini na yenye soko lazima elimu itolewe kwa jamii kuanzia ngazi za chini hadi za juu.

"Jamii iache kufunga ng'ombe kwa stress, ng'ombe anatembea kutoka pori la Karagwe hadi Ngara, kesho wamchinje lazima nyama yake iwe ngumu," amesema Chalamila.
 
Hahaha rc leta amshaamsha

Watu walikumiss

Ova
 
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amewataka wadau wa mifugo kutoa elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji ili kuwawezesha kufanya ufugaji wa kisasa ambao utaepusha ng'ombe kutembea umbali mrefu kutafuta malisho na kusababisha nyama yake kuwa ngumu

Amesema hali hiyo huchangia wafugaji kuendelea kuwa maskini kutokana na nyama kukosa soko.

Akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya wakulima - Nanenane - Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa ili kuhakikisha inapatikana nyama laini na yenye soko lazima elimu itolewe kwa jamii kuanzia ngazi za chini hadi za juu.

"Jamii iache kufunga ng'ombe kwa stress, ng'ombe anatembea kutoka pori la Karagwe hadi Ngara, kesho wamchinje lazima nyama yake iwe ngumu" amesema Chalamila.
 
Mikoa ya mipakani hususan magharibi kwa kawaida wamekuwa wakipewa majenerali. Huyu sijui.
 
Hivi wanapopewa majenerali huwa wanapewa utaratibu mwingine wa kuongoza mikoa , tofauti na Ma RC wengine ?
 
Nyama kua laini lazima uiloweke na viungo...
 
Back
Top Bottom