Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la Mkazi ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 11 hadi 20, 2024 na upigaji wa kura Novemba 27, 2024 ili kuchagua viongozi wa serikali za mitaa.
Wito huo ameutoa leo Septemba 30, 2024 katika Viwanja vya Kilwa Kivinje ambako Kivinje Jogging Club waliandaa bonanza na kualika klabu mbalimbali kutoka mikoa ya Dodoma, Mtwara, Pwani na Dar es Salaam likiwa na lengo la kudumisha afya, ushirikiano, upendo, umoja na hamasa ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.
Aidha, Mkuu wa Mkoa ametoa angalizo kwa wananchi ambao hawana taarifa sahihi kuhusu vitambulisho walivyo navyo na zoezi la kujiandikisha katika daftari la mkazi.
"Wapo wenzetu ambao wanasema tayari wanavitambulisho vya kupiga kura, kwa hiyo hawaoni sababu ya kujiandikisha tena, vile vitambulisho ni kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka kesho lakini kwa uchaguzi huu wa serikali za mitaa, serikali zamitaa, vijiji na vitongoji tunakwenda kujiandikisha kwenye daftari la mkazi," amefafanua Telack.