RC Zainabu Telack: Kasimamieni kwa weledi miradi ya maendeleo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

RC ZAINABU TELACK: KASIMAMIENI KWA WELEDI MIRADI YA MAENDELEO​

Na, Hilarry Shuma OR-TAMISEMI

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainabu Telack, amewahimiza Maafisa tarafa na watendaji wa kata nchini kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao

Akifunga Mafunzo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata, Julai 22, 2025 mkoani Lindi Mhe. Telack amewataka washiriki kuhakikisha kuwa wanakuwa daraja la kuimarisha imani kati ya Serikali na wananchi, na si chanzo cha migogoro.

“Ni jukumu lenu kusimamia amani na utulivu, kuwa karibu na wananchi, kushughulikia kero zao kwa wakati, na kusimamia vyema mapato na miradi ya maendeleo.

"Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza fedha nyingi katika ngazi ya msingi, hivyo hatutegemei fedha hizo zipotee au zisitumike kwa ufanisi,” amesisitiza
Mhe.Telack.

Amewataka Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata kuwa vinara wa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa njia sahihi na za kidijitali, akieleza kuwa ukusanyaji huo ndio msingi wa utoaji bora wa huduma za jamii.

Aidha, amesisitiza kuwa malalamiko ya wananchi yaangaliwe kama fursa ya kujirekebisha, si mashambulizi, na kwamba viongozi wanapaswa kutoa mrejesho wa hoja za wananchi kwa wakati, kwa uadilifu na heshima.

Aidha, Mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) na Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC)

Mafunzo hayo ni sehemu ya mpango endelevu wa Serikali katika kujenga uwezo kwa watumishi wa umma wa ngazi ya msingi, katika kuhakikisha huduma bora na zenye tija kwa jamii.
 

Attachments

  • Screenshot 2025-07-23 at 11-15-41 Instagram.png
    275 KB · Views: 37
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…