Bila hivyo wahalifu hawawezi kusema akiteswa ndipo humpeleka askari kwa washirika wake alikoficha au alipouza..
Mfano makosa ambayo mi nimeshuhudia watu wanapigwa na kuonesha ushirikiano ni Silaha. Huwezi kumuhoji mtu mwenye bunduki kwa maneno tuu criminals hawatoi ushirikiano kirahisi.
Kuna Kesi ya yule mzungu aliyekufa Tanzania 2017 Masaki Aliyekuemo kwenye deal alikua anakaa Majumba sita bunduki ilikua imeifadhiwa kwenye makaburi ya kinondoni lakini kulikua na kipigo ambacho si cha kawaida Bunduki ikaenda kuwa retrieved Makaburi ya kinondoni hawa jamaa walifungwa Kunyongwa hadi kufa.
Iko mifano mingi kuna kesi za mauji ambazo watu wana minywa na kwenda kuonesha maiti zilipo na Polisi wakishakutandika wanajua kama umefanya kweli au unakubali kwa woga tuu. Hii njia ni nzuri kwa wahalifu wengi ni rahisi kujua nani kahusika au nani hajahusika.
Wapo pia wezi wa bodaboda ambapo mara nyingi humuua dereva hawa bila kipigo hawatajani na kusema ukweli.
Kipigo ni muhimu sana katika upelelezi.