Re: Jaman huu utaratibu wa English Medium Schools na Waalim wao Vipi?

Re: Jaman huu utaratibu wa English Medium Schools na Waalim wao Vipi?

Mkuu wangu Frank, hayo ni makosa ya regulatory board, ukaguzi wa shule (unaokufa) aina ya walimu waliopo jatika shule hizi wanatoa notes zao kwenye ma abbot,ma nelkon wanaona hayo ndo wanayopenda wazazi, kama kule kijijini mginjwa akienda hosp asipochomwa sindano. Kazi ipo.
 
Hiyo Mitaala ni formality tuu Mkuu,but ukifanya uchunguzi nini kinachofundishwa huko ndio utajua ninachoongea,kwanza Vitabu vile vya Ithibati na Mazoezi wanavyotumia ni tofauti kabisa na vile vya Serikali,wengi wanatumia Vitabu vya Mitaala ya India na Kenya,sasa hapa Mtoto huyo huyo aje kufanya Mtihani mmoja na watoto wa Shule za St. Kayumba,what did you expect?. Kwenye swala la lugha tuu kiukweli wapo vizuri,kama the Chair,the Table hapo watoto wa Kayumba watasubiri sana but kwenye General knowledge watasubiri sana dhidi ya Watoto wa Kayumba.

Huo ni ufundishaji tu mkuu lakini mbona mtihani unakuwa mmoja tu ila katika lugha mbili tofauti. vipi kuhusu english medium za serikali zinatumia mtaala upi? na kama wanatumia mtaala tofauti kabisa mbona mtihani wa taifa wanafanya mmoja na ufaulu ni sawa tu. Japo matokeo ya lasaba kumi bora nyingi ziliongoza za english medium kama Tusiime, Feza n.k
 
mpeleke shule za kayumba awe anapumzika huko hakunaga ma hworks ni vishert kwa kwenda mbele kazi ni kumpa mfagio na dumu la maji

asikudanganye mtu nchi nyingi za kiafrika elimu yetu ni ya kukalili tu wewe huwezi kusoma masomo kumi na moja na ukaelewa yote


kama mtoto hafanyi home works kibongobongo hawezi toka kumbuka watoto hawana muda wa kujosomea kiumri na kiakiri kulingana na umri wao wa michezo

kama unabisha fanya haya

nenda shuleni kwao uwaambie walimu wasimpe mtoto homeworks then usimwambie kusoma uone :wanamichezo mia kwa siku hawa jamaa

Jamani hapa sidhani kama ni suala lakusema mpeleke shule za Kayumba. Kwanza Dhihaka hazijengi. Kikubwa hapa ni kuangaliahoja ya mtoa mada. Kwani kama kweli watoto wanapelekeshwa na ma- home work yanayopita kiwango si afya kwamtotovilevile.Pamoja na kupenda watoto wafaulu lakini sijui kama kukarirsha maswali na majibu ni vizuri. Sijui pia kama kuwafundisha watoto kiasi kuwa hawapati muda wakupumzikani vizuri pia.

Kwa upande wangu sina hakika kama Wizara husika inafuatilia vya kutosha hizi shule kwa kweli kwani nyingine ni majanga. ada kubwa kupita kiasi, na ada hiyo ndiyo inayojenga shule sidhani kama hii ni sahihi!! Wakati juhudi za kuhakikisha shule za (baadhi wanazozikebehi) ambazo kwa kweli zina curriculum nzuri ufuatiliaji ndio tatizo. Wizara ifanye juhudi ufuatiliaji wa shule hizo za public zirudie ile hadhi ya zamani jamani. Nakumbuka nilivyochaguliwa kujiunga Forodhani Secondary Shool, DSM shule ya public nilivyofurahi.Wakati huo huo shule za Binafsi zifuatiliwe pia sio tu viwango bali hata namna ya utoaji wa elimu kwa watoto kwa ajiliya afya ya kimwili na kisaikolojia pia. Waangalie elimu itolewe kwa kiasi kinachoendana na umri wa mtoto kwa kweli.

Kuna mifano ya shule kama 'Agakhan' nayoifayamu miaka ya 90s , mtoto anapata best education, anapata muda wakucheza, kupumzika, kuwa oriented katika kuweza kujisomea vitabu nk.
 
Mi wa kwangu anaenda shule saa 2 hadi 5 na nusu au 6 kesharudi. Na homeworks wanapewa Fri hadi Fri. Huyo wa nursery.
Na nijuavyo mimi hao wanochelewa kurudi wanakula na kulala huko huko shuleni. Wanacheza pia.
 
Mi wa kwangu anaenda shule saa 2 hadi 5 na nusu au 6 kesharudi. Na homeworks wanapewa Fri hadi Fri. Huyo wa nursery.
Na nijuavyo mimi hao wanochelewa kurudi wanakula na kulala huko huko shuleni. Wanacheza pia.

Na huo ndo ukweli ila wengi wanaosema hapa inaweza kuwa wazazi lakini wale wasiofatilia maendeleo au ratiba za watoto wao mashuleni.Hakuna shule inayorudisha mtoto jioni bila kulala na kucheza hao wakiwaona kwenye vischool bus jioni wanarudi wanadhani since morning walikuwa class tu kitu ambacho sio kweli.
 
Yaonekana wazi una chuki tu na hizi shule za English medium na wala si uhalisia unaouongea, huwezi ukawa serious kudai kwamba hawa watoto wa English medium wanazidiwa na hao wa Kayumba kinadaharia tu bila kuwa na ushahidi wa hicho unachokiongea, takwimu zipi unazotumia wewe kusema hayo?
Acha kupotosha, ukweli upo wazi kwamba shule hizi za English medium zina kiwango bora cha elimu ukilinganisha na hizo za kayumba. japo zipo chache zinazoongozwa na Makanjanja wa elimu mimi siziweki lakini nyingi ni nzuri kupita hizo za kayimba unazozizungumzia. Usitake kupotosha hapa
 
Hizi Shule ni pasua kichwa kabisa na nadhani ni Msiba na Janga jingine kwenye mfumo wa Elimu yetu hapa Tanzania. Kwanza masomo wanayofundishwa utakuta hayaendani na level yao ya kidarasa na kiakili,imagine Mtoto wa STD five ameshasoma na kumaliza ile Topic ya Reproduction ya form three sasa sijui hapa kuna faida gani?. Pili hizi shule kwa outings za kwenda sijui Beach na Mbugani ndio zinaongoza. Tatu watoto kupewa H/W zilizo juu ya uwezo wao,utakuta Mtoto amepewa H/W ya masomo 3 na zote hazipungui uchache wa maswali 20 kwa kila somo na kilichoniacha hoi ni pale Mtoto alipopewa H/W ya swali moja then jibu la hilo swali alirudie kuliandika mara Mia Moja,sasa hapa ni kumfundisha Mtoto au kumkomoa?

Mimi nashauri Serikali iingilie kati kwa hili hasa kuhusu Mitaala wanayotumia hawa watu,kwanza utakuta Shule inafundisha Asilimia 95 kwa kutumia lugha ya Kiingereza na Kifaransa,wakati kwenye Mitihani ya Taifa i.e STD na Seven lugha inayotumika kwa Asilimia 95

Ni kweli mkuu,maana ukiangalia masomo ya mwanafunzi wa darasa la tatu ni form two.
Yaani majanga matupu,maana hata akifika huko form two hana hata moja,na mbaya zaidi zimekuwa hazifanyi vizuri sana maana wao wanarukia topics za mbele kuliko mtu anachoenda kufanyia mtihani wa taifa kinakuwa chini ya uwezo wake.
 
Acha ujinga wewe,Watoto kuwa overloaded na H/W na masomo kuliko saizi yao na kusoma hizo shule za English Medium ndio mfumo wa Elimu kukua?hizi zero zinazongezeka kila Mwaka kwa form 4 na watoto kwenda Form One pasipokujua kusoma wala kuandika ndio mfumo wa Elimu unakua?mbona hizo English Medium haziongozi au kufanya vizuri kwenye Mitihani ya Taifa ya Darasa la Saba zinazidiwa na Shule za St.Kayumba.

Hili nalikubali,Kayumbas zinawakimbiza sana kwenye Darasa la saba
 
Back
Top Bottom