Kabaridi
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 2,022
- 534
- Thread starter
-
- #21
Hapana mzalendo jaribu kutuelewa kuwa hatutaki kuintergrate kwasababu hatujajiandaa vya kutosha na sio kwasababu tuko self sufficient. Kabla hatujaingia tunataka tujue kama nia yenu wakenya ni mbaya au nzuri, maana tunajua kuwa pamoja na kuwa kulikuwa na sababu nyingi zilizopelekea kuvunjika EAC mwaka 1977 lakini ni kenya iliyokuwa ya kwanza kuvunja jumuiya sasa kwanini sasa hivi mko mstari wa mbele kutaka intergration? Kenya wanafahamika kwa kuwaabudu wazungu kwa miaka mingi kuliko Tanzania sasa kwanini sasa mmegeuka ghafla na kujifanya mnajali zaidi maendeleo ya Africa Mashariki? Sasa wakati tunaendelea kutafuta ukweli nyie wenye haraka endeleeni tutakutana baadae na kama tukikuta milango imefungwa tutaendelea na SADC yetu ambako hatuna wasiwasi na mwanachama yeyote. Kama intergration inalipa kwanini kila mwanachama atulalamikie sie wakati kuna nchi zingine zimefungua mipaka? Wanaoona TZ kuna vikwazo vingi kwanini wasifanye biashara ktk nchi zilizofungua mipaka mpaka pale TZ itakapofungua i.e kama Rwanda na Kenya zimefungua mipaka kwanini watu wasifanye biashara kati ya nchi hizo huku wakisubiri nchi zingine nazo zifungue.
Kila nchi inajua itafaidika vipi na intergration, sie watanzania tunafaidika na jumuiya yenye ushindani lakini sio kuungana kijumla jumla tu. Tunajua tumekosea wapi mpaka tukawapa upenyo wakenya sasa tunataka turekebishe kwanza halafu ndo tuendelee na siasa za kufurahisha umati.
We Kibona it seems you hate your life. Unaongea juu ya SADC. Just rethink because you will be burnt while walking on the streets of SA. Zimbabwe felt the full wrath of the SA population.