Re:sakata la mitaala rasmi

Re:sakata la mitaala rasmi

blauzi

Member
Joined
Aug 28, 2008
Posts
24
Reaction score
5
Naanza kufanya utafiti juu ya suala la mitaala rasmi

Kutokana na sakata lililoibuliwa na Mh. James Mbatia (Mb) kuhusiana na suala la mitaala (Kama Tanzania kuna mitaala rasmi au la) nimeamua kuanza kufanya utafiti juu ya suala hilo na nitakuja na ripoti (Simaanishi hakuna tafiti zilizokwishafanywa, zipo nyingi mno)

Hadidu za rejea
1.Mtaala ni nini?
2.Wadau wa elimu wanaupa dhana gani mtaala
3.Uelewa wa wanaopigania suala la mitaala ukoje
4.Uelewa wa watendaji wa serikali juu ya dhana hiyo ya mitaala ukoje
5. Uelewa wa wabunge (akiwemo Mh.Mbatia) juu ya suala la mitaala ukoje
6.Uelewa wa waziri wa elimu juu ya dhana ya mitaala na naibu waziri wake
7.Nyaraka gani iliwekwa mezani na waziri mwenye dhamana (iliyowasilishwa mbele ya wabunge) walipoikomalia serikali kuwapa mtaala rasmi

Kwa kuanza, mwenye hiyo nyaraka(document) iliyowasilishwa mezani kwa Mh.Spika ati ni mtaala anitupie inbox tufanye kazi. Matokeo ya utafiti wangu nitakuwa nayatoa hapa bure kwa vipande vipande.Asanteni sana
 
Back
Top Bottom