Nimekupata. Kweli kabisa huwezi kutumia ubongo pekee bila kushirikisha mwili, ila sikumaanisha hivyo: Umewahi kusikia au kuona watu wanatumia mwili zaidi ya ubongo vyuoni na makazini ili kujirahisishia/kuweka njia nyeupe? sasa hayo yapo na kuna mabosi wanaendekeza hayo. Hope umenipata vilivyo nini namaanisha.
Hongera kwa kupata kazi na kushiriki nasi katika kutupa ushuhuda. Je umeolewa? Nahisi nimeanza kukupenda ghafla.
Wapendwa Sina jinsi ya kuielezea furaha yangu. Nimekuwa member wa JF kwa takriban mwaka sasa. Mie huwa si msomaji wa magazeti, na taarifa nyingi muhmu huzipata kupitia hapa JF. Kwa mara ya kwanza hii forum imenisaidia na nimeyaona matunda yake.
Nimefanikiwa kupata kazi, amabayo kwa mara ya kwanza niliiona hapa JF, katika forum ya "Nafasi za Kazi na Tenda". Mwanzoni sikuamini kama nami naweza pata kazi serikalini bila kuwa na mtu wa kunishika mkono, lakini leo imewezekana. Ni kweli kuna uwazi na ukweli na usawa kupitia Sekretariatiya Ajira na Utumishi. Tuliitwa watu saba na nafasi ilikuwa moja tuu.
Nimepata,
Namshukuru Mungu na WanaJF, Tuendelee kulijenga Taifa letu. Big up JF, LIVE LONGER.
Kwa wengine, Msikate tamaa, endeleeni kuomba kazi bila kuchoka, ipo siku mtafanikiwa, na tusipuuze kazi, na tufanye kazi kwa bidii na kutumia nafasi zetu kwa manufaa ya umma.
Asanteni.
Hongera sana mwanangu kupata kazi na kukumbuka kumshukuru Mungu kwamba yeye pekee ndiye ameruhusu kwa wakati wake muafaka umepata kazi
Wahi kazini na waheshimu wakubwa wako utapata mafanikio na upatapo mshahara usisahau kurudisha fungu la kumi la mapato yako utabarakiwa
Pia umefanya vyema kuwashukuru pia JAmiiforums nasi wanachama wenzio tumefurahi. Mimi binafsi nina mambo kazaa ninawashukuru jamii forums nimefanikiwa kadhaa
Lol, Nimeipenda hii Post ghafla. wacha nkaoge nibadilishe na nguo, niweke makeup, then ntakuja rasmi kuijibu tehe
hongera sana. hakika umevuka kikwazo kimoja (kutafuta ajira), naamini
vikwazo utakavyovikuta huko uendako utavikabili kwa mtazamo chanya
na kuvivuka bila wasiwasi,
Hongera kijana, fanya kazi kwa bidii huko serikalini usaidie kupunguza urasimu usiwe na wewe mmoja wa wale wanaonyanyasa wananchi unafika asubuhi hadi saa tano unasoma magazeti wakati sisi tumepanga foleni toka saa moja asubuhi tunahitaji huduma.
Hongera
Wapi wewe mfanyakazi wa sekretarieti unajifanya umepata kazi.Sema unataka uwaosheee nenda Fb huko kawadanganye wenzio sio hapa
kweli akili ni nywele,...... badala ya kusema mshahara wa kwanza anunue vocha mojamoja za mitandao tofautitofauti na awe akiziweka katikati ya mada yoyote mpaka ziishe, wale wanaosoma na kufuatilia mada za JF watafaidi kila mtu kwa kadiri ya anavyojituma kuitumia JF. :dance:Hongera sana, inabidi mshahara wa kwanza tukajengee heshima bar sawa?