Asante my dear
paesulta, ni kweli sikudhani kuwa mtoto wa mkulima mie ningeweza kupita katika tundu la sindano, kwani nilikuwa najaribu bahati yangu. Cha muhimu ni kuzingatia maelekezo yaliyotolewa katika tangazo la kazi, uandishi mzuri wa barua ya maombi ambayo iko wazi, CV iliyopangiliwa vizuri, na viambatanisho vyote vinavyohitajika.
Pili kwenye intavyuu, kujiamini kunahitajika, haina haja ya kujisomea saaaana, ila kujiamini na kutulia. Ukweli ni kuwa PANEL inatisha especially kama mtu hajazoea maintavyuu. Ingawa ukitulia na kujibu kwa utulivu una advantage sana.
Tatu, usiache kujibu swali hata moja, wala usiseme sijui, jaribu kujibu tuu kulingana na uelewa wako, usizunguke swali nenda direct kwenye pointi.
Kwa mara nyingine Naipongeza Tume ya Ajira, kwa usawa huu.