Hii sector inahitaji akili zaidi kuliko pesa. Akili ya kuangalia value ya kiwanja, nyumba au frem ya biashara kwa miaka kama mitano au kumi ijayo.
Real estate ya Tanzania awali ya yote usiifanye ki proffessional sana. Achana na mambo mortgage, sijui ma engineer etc. Ukienda ki proffessional utashangaa nyumba ya million 30 umeijenga kwa milioni 70.
Kitu kikubwa anza wewe kama wewe hata kama una mtaji wa milion 20 soma mazingira tafuta hata vile viwanja vya 3,000,000 ingia hapo same chukua mafundi wa bei chee room moja gharama za ujenzi hata 120000 wanakufanyia. Wewe kwa kitu kama 15,000,000 unajenga room zako nne safi za biashara. Hapo ukipiga rent 70000 kwa mwezi kwa mwaka ni kama 3.3 M hizo unazuchukua paaaap unanunua uwanja mngine.
Kama umeajiriwa ukipata salary ya miezi mitatu hapo ni tofali kama 3000 mwezi wa nne ni cement na mchanga mwezi wa 5 hela ya mafundi na ujenzi unaanza.
Ki ufupi tu kama alivosema mdau hapo itakuchukua mda mpaka uje kuona matunda ya uwekezaji huo. Lakini kama upo organised na determined ndani ya miaka 6 au 7 unaweza kuwa tayar na real estate worth 100 million.
Mi kuna mahesabu ya ujenzi nnayo nikiwaambia watu unaweza jenga nyumba safi kwa m 30 watu wanabisha kabisa. Coz hivo vitu havipo kwenye fikra zao. Wao wakisikia nyumba basi mawazo yao ni M 100.
Sasa ndo ujiloge ujenge nyumba ya milioni 100 kwa mortgage halafu utegemee kuirudisha kwa kupangisha... Hahahahahh.. Mbona utaweza kuzaa na benki. Kwanza real estate haihitaji nyumba za luxury. Unaweza ku design chumba sebule choo jiko halafu uweke sokoni kwa 30 M hapo bado ni faida tu. Kwa mwaka ukiweza ku develop nyumba kama hizo simple hukosi 10 M faida kwa kila unit.
Hata Trump kuna sehem aliandika kama huna mentality ya penny pinching au cost minimization Real Estate itakuwa kitu kigumu sana. Na ndicho naona kina gharimu watu wengi mpaka kesho
So real estate ni mentality zaidi kuliko pesa