Nashukuru sana chief kwa kuchukua muda wako na kuandika haya muhimu nitayafanyia kazi, haya niliojifunza na sita sita kukusumbua pale nitakapokwama nipate ushauri zaidi hii ni ndoto yangu .
Kwa sehemu ipo ni maeneo ya kijitonyama nimefanya utafiti nikaona mji unakuwa sana ukianzia victoria kuja makumbusho new offices ni nyingi ,kwahiyo vijana wengi professionals wataitaji kuishi karibu ndio target market yangu napia unaona NHC wanajenga apartments zao but bei zao kidogo nikubwa kwa vijana wanaonza kazi sidhani kama they can afford .
Na nataka nijue ninapoenda bank watataka kuona business proposal kwanza au watatuma valuers wao waone eneo nakuamua wao watatoa how much?
Na suala la michoro ninaweza kuwatumia hawa vijana fresh from chuo nadhani gharama zao sio mbaya kama hawa wengine ambao wazoefu na bei zao ni zoefu pia?Na pia hao Qs?
Engineers inabidi wenye uzoefu maanna isiletekizaazaa kwenye ujengaji
Mkuu nimerejea labda nieleze kwa kifupi juu ya masuala machache uliyoyataja;
Swala la Ofisi Kijitonyama.
Hili kwa sasa ni eneo zuri kwa kujenga ofisi kwa kuwa kuna node imeanza kuota maeneo hayo. Ni vema kuzingatia pattern ya office properties ya eneo husika. Eneo lile ofisi property zinaegamia barabara kubwa ya Al~Hassan Mwinyi natumaini nawe eneo lako lipo usawa huo. Kujenga jengo la Ofisi mbali na barabara hiyo kunaweza kukuathiri hasa kama utajenga upande huu ndani wa eneo la Makumbusho kwa kuwa eneo hilo kwa kadili unavyoenda mbali na barabara kuu lina miundo mbinu mibovu na linazidi kujitenga na ofisi nyingine kitu ambacho si kizuri. Majengo ya ofisi yanafaa yawe karibu karibu kwa kuwa huduma zinategemeana kati ya ofisi moja na nyingine.
Kuna risk kubwa ya kuangalia hapa. Iwapo serikali itaamua kuhama kweli kutoka Dsm, majengo mengi ya katikati ya mji yatakuwa wazi. Hivyo kuna uwezekano ofisi nyingi za pembezoni mwa mji hasa hapo Kijitonyama wakarudi Posta. Iwapo watarudi, majengo mengi hapo yatakosa wapangaji na wewe ambaye ndie kwanza umejenga unaweza kujikuta kwenye wakati mgumu.
Kama utajenga nyumba za kuishi (eg apartments) kuna hitajika umakini mkubwa. Wateja wengi wa apartments sio graduates wa chuo wala waswahili ni professionals kama ulivyosema. Ila kama umefanya research utagundua biashara ya apartments nayo imeanza kuyumba. Bei za kupanga na kununua zimekuwa changamoto kwa Watanzania wa kawaida.
Watanzania wenye hali nzuri kidogo na foreigners ambazo ndio wadau wakubwa nao ni kama wameanza kuwa wachache ukizingatia supply ya properties mpya.
Hata hivyo kama utaweza kumarket vema bidhaa yako na kuibrand vizuri soko bado lipo.
Swala la Mikopo Bank
Bank watahitaji vyote collateral na business proposal kwa kuwa pesa ya kudevelop property sio ndogo. Kwa mantiki hiyo watafanya valuation ya mali unayoweka kama collateral ili kujua unakopesheka hadi kiwango kipi. Pia kama ni mkopaji mzuri bank na una biashara nyingine unaweza kukopesheka zaidi juu ya kiwango cha collateral yako.
Bank tofauti zina sera na riba tofauti. Ni vema ukatafiti hasa riba na masharti ya kila bank kabla hujaamua kukopa bank yoyote.
Swala la kutumia vijana ni cheaper option ila ina complications zake. Kuna swala mathalani la vibali, mfano Architect kwa project unayokusudiwa lazima awe amesajiliwa, QS na Engineer vilevile ili upate vibali vya ujenzi.
Hata board husika nazo hufanya ukaguzi wa kushtukiza kuangalia kama engineer amesajiliwa au la.
Lakini hili si kusajiliwa si kikwazo zipo namna za kutatua changamoto hizo. PM kujua unavukaje hapo.
Kuhusu bei mara nyingi QS ni 2% ya gharama ya mradi na Architect huwa 3~5%. Hata hivyo hizo bei ni muongozo tu, bei halisi hukubaliwa kwa majadiliano.
Mkuu nakutakia kila la heri katika kudevelop property yako.