Real madrid fc wamepotezewa muelekeo?

Real madrid fc wamepotezewa muelekeo?

mpingauonevu

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
621
Reaction score
433
Hatimaye Barcelona imerudi kwenye mbio za ubingwa baada ya mfulululizo wa Madrid kutoa suluhu. wakati jumapili walitoa suluhu ya 1-1 na malaga kwa free kick ya dakika za mwisho leo pia wametoa suluhu na Vilarreal ya 1-1 tena kwa free kick ya Marco Senya ya dakika ya 83 kurudisha goli maridadi la christiano Ronaldo.

Yaliyojiri uwanjani
Kama ingekuwa ni YANGA huyu refa wa leo angefia uwanjani! ni wazi alikuwa anachezesha mechi kwa masilahi ya Barcelona! Alianza kumtoa nje msaidizi wa Morinho(sijamshika jina). Baadae akampa sergio ramosh yellow ya pili! wakati Madrid wanajipanga kuikubali red card ya Ramosh, Ozil akalimwa direct red card, morinho na yeye akalimwa red wote tukabaki tunashangaa.kwa nini nasema mazingira yalikuwa ya kuinufaisha barcelona? tunajua mfumo wa morinho ni wa kutumia nguvu lakini kwa jana waloiokuwa wanacheza vurugu ni villarial. Morinho anajitahidi sana kuepukana na fujo siku hizi ndio maana hata mechi ya jana baada ya ramosh kupewa red card hakulalamika sana wala hakukuwa na vurugu.

Tunajifunza nini?
Madrid hata walipokuwa pungufu kwa watu wawili hawakulalamika saana na kandanda waliyoonesha dakika zingeongezwa wangeweza kupata bao la pili.Timu zetu za Tanzania zinapaswa kujifunza hili. Ukomavu wa wachezaji ni pamija na kuvumilia unachohisi ni hujuma kwa faida yako mwenyewe na kwa timu. shida ya wachezaji wetu wanacheza kwa nguvu ya bangi na bangi haijawahi kuonesha kiwango cha kutosha cha uvumilivu.
 
Madrid nao wamezidi.Hata mimi niliangalia ile mechi ya jana.Ozil alimtukana refa,Ramos alicheza rafu mara kwa mara.Mourinho na msadizi wake walitoa lugha chafu kwa waamuzi wa akiba na refarii.Walistahili kuadhibiwa kwakweli.Barcelona hawahusiki Mkuu..
 
kutangulia si kufika, kumbuka kituko alichofanya simba sports club mwaka jana, alioongoza ligi vizuri kabisa akijulikana atakuwa bingwa wapi akaja kukoroga, Liverpool hvo hvo kuna mwaka hivi karibuni alikalia kitu muda mrefu, aliboronga, Man U akachukua ubingwa kilaini, tuje kwa Man city ameongoza ligi kitambo, anaanza kupumuliwa na kuwekwa chini na yule yule man U, SASA HALI HII NAIONA KWA REAL MADRID, lets wait and c
 
Madrid nao wamezidi.Hata mimi niliangalia ile mechi ya jana.Ozil alimtukana refa,Ramos alicheza rafu mara kwa mara.Mourinho na msadizi wake walitoa lugha chafu kwa waamuzi wa akiba na refarii.Walistahili kuadhibiwa kwakweli.Barcelona hawahusiki Mkuu..

Lugha chafu uliisikia ? Mwenzetu una uwezo wa kusoma lugha ya lips either ni Kireno au Kispanyola. Uko juu wangu
 
Piga,ua,garagaza........Bingwa wa La Liga 2011/2012 ni Real Madrid.....
 
Hii ligi bado ipo open kumbuka Barca anapoint 3 kwenye mechi dhidi ya Real Madrid
 
madrid bado ipo juu sasa hv imeshailiza team ya RSO 5 kwa 1 dk ya 65
 
I hate barcelona, but madrid hii haihaminiki, natamani twende nou camp for el clasico huku tunaongoza kwa point 10 and above, sababu pale lazima tutafungwa tu labda messi asicheze,
Tatizo madrid tuna panic sana hasa tukipata kadi au tukizidiwa, nimecheki game ya barca leo wamepata red card mwanzon mwa mechi lakini wametulia hakuna kulalamika wala nini na wanagonga pasi kama wako ishirini nikajua kabisa nou camp itakuwa balaa kama tukienda na gape la 3 point sababu ndo tutawapelekea ubingwa barca sababu watatufunga tu na ligi ya spain haiangalii magoli mengi mkiwa na point sawa wanaangalia nani kamfunga mwenzake,

I am a madrid fan but I am sure bado hatujawa na team ya kuifunga barca kwa kuizidia zaidi ya kubahatisha as mpira unadunda, na nou camp sitegemei ushindi kabisa
 
Back
Top Bottom