mpingauonevu
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 621
- 433
Hatimaye Barcelona imerudi kwenye mbio za ubingwa baada ya mfulululizo wa Madrid kutoa suluhu. wakati jumapili walitoa suluhu ya 1-1 na malaga kwa free kick ya dakika za mwisho leo pia wametoa suluhu na Vilarreal ya 1-1 tena kwa free kick ya Marco Senya ya dakika ya 83 kurudisha goli maridadi la christiano Ronaldo.
Yaliyojiri uwanjani
Kama ingekuwa ni YANGA huyu refa wa leo angefia uwanjani! ni wazi alikuwa anachezesha mechi kwa masilahi ya Barcelona! Alianza kumtoa nje msaidizi wa Morinho(sijamshika jina). Baadae akampa sergio ramosh yellow ya pili! wakati Madrid wanajipanga kuikubali red card ya Ramosh, Ozil akalimwa direct red card, morinho na yeye akalimwa red wote tukabaki tunashangaa.kwa nini nasema mazingira yalikuwa ya kuinufaisha barcelona? tunajua mfumo wa morinho ni wa kutumia nguvu lakini kwa jana waloiokuwa wanacheza vurugu ni villarial. Morinho anajitahidi sana kuepukana na fujo siku hizi ndio maana hata mechi ya jana baada ya ramosh kupewa red card hakulalamika sana wala hakukuwa na vurugu.
Tunajifunza nini?
Madrid hata walipokuwa pungufu kwa watu wawili hawakulalamika saana na kandanda waliyoonesha dakika zingeongezwa wangeweza kupata bao la pili.Timu zetu za Tanzania zinapaswa kujifunza hili. Ukomavu wa wachezaji ni pamija na kuvumilia unachohisi ni hujuma kwa faida yako mwenyewe na kwa timu. shida ya wachezaji wetu wanacheza kwa nguvu ya bangi na bangi haijawahi kuonesha kiwango cha kutosha cha uvumilivu.