SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kuna wakati unasikiliza baadhi ya watu huku mitandaoni unabaki kujiuliza hawa watu wanaujua kweli mpira au naongea na bots (kwa wasiojua bots ni mifumo ya kicomputer inayoact kama binadamu mitandaoni ikiwemo kupost comments).
Mambo mengi ambayo tunashadadia ni ya kawaida sana kwenye ulimwengu wa mpira. Timu kubwa inaweza kutandikwa goli za kutosha hadi ukashangaa. Timu ndogo sana usiyoitegemea inaweza kuifunga timu kubwa bila mtu yoyote kutarajia. Ndiyo ni mambo ya kushangaza ila yakitokea siyo mara ya kwanza na siyo ishara ya kiama!
Kuna hili limeibuka baada ya mechi ya Al Ahly Tripoli vs Simba, ambapo watu wanaonyesha kushangaa hadi wengine wanafikiria kuweka mabango kisa Simba imeshindwa kupata shot on target hata moja katika mechi nzima.
Nikiweka mfano mmoja wa haraka, ni mwaka jana tu hapo 2023 wala siyo mbali, Real Madrid akicheza nyumbani dhidi ya Barcelona walifungwa 0-1 na wakamaliza mechi bila kuwa na shot on target hata moja. Real Madrid ilikuwa full mkoko, Vinicious, Modric, Benzema, Camavinga, nk. wote ndani.
Mambo kama haya yakitokea unaweza na unaruhusiwa kushangaa ila usipitilize sana, mbona yanatokeaga sana tu? Kwanza kutokuwa na shots on target haimaanishi haukufika langoni mwa mpinzani na haimaanishi haikufanya attempt yoyote ya kufunga dakika zote 90, ni kwamba katika mashuti yote na vichwa vyote mlivyopiga hakukuwa na hata moja lililokuwa target ndani ya milingoti ile 3. Nothing more nothing less. Ukielewa hivyo wala hautawaza saaana.
Jifunzeni mpira nyie bots.