Real Madrid wana gundu na wachezaji wa Chelsea

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Kiukweli tokea Real Madrid wamsajili Curtois (sijui jina nimepatia?) Real Madrid imekuwa ikiruhusu magoli ya hovyo sana kupitia huyu kipa; naona laana ya mashabiki wa Chelsea inafanya kazi kwake lakini hata ukimuangalia Eden Hazard, ingawa aliondoka kwa amani Chelsea, lakini kiwango chake ndani ya Madrid hakiridhishi na umri unazidi kwenda. Hazard wa Chelsea na team yake ya taifa, Belgium, si huyu wa Madrid.
 
Hakuna golikipa pale! Lile ni pazia. Hakuna ujinga alioufanya Zidane kama ule wa kumuachia golikipa mkongwe na aliyeipa mafanikio Real Madrid kwa misimu kadhaa Keylor Navas kwenda PSG!

Ila Madrid na yenyewe ina wababu wengi waliopitwa na wakati. Sergio Ramos hana jipya, Rafael Varane hana jipya, Marcelo naye amekuwa kama yule marcelo mwenzake wa Yanga! Beki 2 naye wa jana alikuwa ni kama Haruna Shamte wa simba!

Kiujumla timu ina wakati mgumu kwa misimu miwili mfululizo bila ya Christiano Ronaldo.
 
Zidane siyo kocha; achana na zile UEFA za ujanjaujanja. Watabomolewa mpaka watajuta, watamfukuza tu.
 
Hahahaha! Zidane huyu ni kama kocha fulani hapa Bongo.
 
Real wanakoseaga kwenye sajili nyingi za pesa nyingi.
 
Mbona mapema mnaanza kunung'unika subirini bado vipigo vinawafata vya kutosha[emoji23]
 
Cortous tangu alipofungwa magoli ya tobo na Lionel Messi ndio alipoteza confidence jumla
 
Huyo walimsajili sijui kwa vigezo gani. Sijui urefu, sijui kitu gani. Jamaa ni pazia aisee, wanatamani kimrudisha kipa Navas ambaye walimnyanyasa kila msimu wanataka kuleta kipa wakati yeye ndiye anawabeba
 
Yule Marcelo ndio kwisha kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…