Kiukweli tokea Real Madrid wamsajili Curtois (sijui jina nimepatia?) Real Madrid imekuwa ikiruhusu magoli ya hovyo sana kupitia huyu kipa; naona laana ya mashabiki wa Chelsea inafanya kazi kwake lakini hata ukimuangalia Eden Hazard, ingawa aliondoka kwa amani Chelsea, lakini kiwango chake ndani ya Madrid hakiridhishi na umri unazidi kwenda. Hazard wa Chelsea na team yake ya taifa, Belgium, si huyu wa Madrid.