Wote ni watu wenye pupa na wamefanya maamuzi yaliyoigharimu serikali ambayo yanajulikana wazi.
Sitaki kuegemea kuongelea tetesi na tuhuma zisizo na mshiko wala dira.
Je usimamizi wao wa Ki-uwaziri wa fedha na bajeti ulikuwaje? Je Ripoti za CAG ambazo huonyesha ukaguzi wa mahesabu ya Wizara yanaweza kutupa sura gani ya uwezo wa hawa wawili kuwa wasimamizi wazuri wa fedha, bajeti na matumizi?
Je kama (kwa mfano) mwaka wa ripoti 2006, ofisi ya Waziri Mkuu au Wizara ya Ujenzi ilionekana kulikuwa na matumizi au upotevu wa fedha Shilingi laki 2, je kama mawaziri, walifanya nini kutokana na taarifa hizi za ubadhirifu?
Je kama mwaka uliofuatia, ikaonekana kwa mwaka mwingine wa fedha sasa zimepotea laki 8, je waliwaita PS na msimamizi wa fedha? je walipeleka barua au maelezo gani kwa mkaguzi mkuu au hata kwa Bunge na Raisi kuhusiana na upotevu na matumizi haya yasiyoidhinishwa?
IKiwa mwaka wa tatu ripoti bado inaendelea kugonga nyundo sasa zimepotea Milioni 5 na hakuna stakabadhi au ni wazi watu wamefoji stakabadhi na kupika vitabu, walijieleza vipi kwa Rais?
Kwa kuwa ripoti kama hii ni public na factual na wote wanajidai wanaweza kusimaia uchumi na fedha ya nchi isitumike ovyo basi tuanzishe ka-jedwali ka mwaka hadi mwaka tuangalie na kupima kama wana umakini kwa wanayoyasema leo wakitaka usimamizi mkuu wa nchi nzima!