Rebecca Gyumi na skendo ya kuiba wazo la Mwanamke Initiative

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072
Mwanaharakati na Mwanajamii, Rebeca Gyumi, ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative anayefanya shughuli zake kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali ikiwemo Umoja wa Mataifa (UN), amenasa kwenye skendo chafu baada ya kudaiwa kuiba wazo la kundi lake alipokuwa akifanyia kazi awali, TAMWA.



Mdau ambaye amewahi kushirikiana na Rebecca kwenye taasisi hiyo isiyo ya kiserikali, anadai wazo la Mwanamke Initiative lilibuniwa na team yao ambapo nguvu, juhudi na maarifa makubwa yalitumika na kila mwanakundi kuwa na matarajio makubwa kupitiamo, lakini kwa ubinafsi na 'ujanja wa mjini', binti huyo aliwazidi kete wenzie na kuchakachua proposal iliyoandikwa kisha kujinufaisha nayo binafsi.

Kama taarifa hizi ni za kweli, basi wizi huu wa kitaaluma sio sahihi na wenye tabia kama hizi waache kwa maana kunaua ndoto na morali ya washirika wenza..

Inawezekana kukawa kumefanyika kosa la kiufundi la "kuaminiana" kulikopitiliza ambako kulipelekea washirika wasisajili wazo hilo.. Iwe funzo.
 
Hata Professor Janabi ambaye ni Director wa Cardiology pale Muhimbili alishawahi kuibiwa paper lake kule Japan na "mjapan"

Haya mambo kwenye fani yapo, japo ni upuuzi wa hali ya juu. Wenzetu wanachukulia serious sana neno "Plagiarism".

Lakini pia waafrika tuna shida ya kutodocument maandishi na hasa kwenye mikutano.
 
Ujanja ujanja wa mjini
 

Kama wazo limeshamtoa samehe x 70. Tuangalie jinsi ya kufaidika kitaifa/ kibinafsi na fursa aliyoipata. Lisiwe sasa tukose wote !! maana UN wako makini sana na uporaji wa kitaalamu. Kuna Mama mmoja alirudisha nyumba baada ya kushtukiwa kuchukua mali za maskini wakati yeye alishaula huko majuu. Wivu wa XX, Mbona naye alichangia mawazo yake kwe hilo kundi?
 

Inasikitisha sana. Hapo kwenye bold ni muhimu sana mkuu.. We take things for granted!
 
Mnamsingizia tu dada wa watu kwanza hajawahi fanya kazi TAMWA
 
Naikumbuka mwanamke initiative tangu rebeka anapita pita kwenye maofisi yetu kuomba omba michango asaidiwe kupanga ofisi. Hawakumuona wamdhibiti?
 
Mkuu ushahidi uko wapi mbona unataka kumchafua dada wa watu
 
Km huwezi kupambana naye,jiunge naye
 
Knowledge is, at best....stolen! So mwacheni Rebecca!
 
mweee nchi hii nilishangaa kusikia chupi zinaibiwa, sasa mawazo yanaibiwa.... mtatuibia hadi hamu ya kupuuuu jamani mweee..... punguzeni wizi
 
Wanaharakati wa kuunga-unga wameishiwa pumziiiii na pozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…