Tukiwa tumetoka kusherehekea kuzaliwa kwa Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Tunasherehekea mwanzo wa Safari ya ukombozi wetu.
Yesu ametufunza upendo na heshima kwa viongozi wetu, Kiimani mimi mi Mkristo wa kanisa la Kilutheri. Ninaheshimu misingi na Miongozo ya kanisa langu.
Leo nimepita katika Mitandao ya kijamii kuperuzi na kuona yale yanayoendelea Duniani nilikutana na Taarifa kutoka katika mtandao wa Zamampya ambayo ilikua ikitoa habari aliyotoa Askofu wangu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania Askofu Shoo akiwasihi vijana kuhusu kupunguza kunywa pombe.
Kwangu mimi taarifa hii ni faraja kubwa na ni Tiba kwetu vijana kutoka katika kinywa chenye hekima kwa kanisa. Kilichonifanya niandike andiko hili ni Majibu ya Binti asiye na nidhamu katika nchi hii, Binti aliyeshindikana na kila mtu, Binti ambaye mpaka sasa haijulikani ni viongozi gani wamlinda asiguswe kwa huku akiendelea kudhalilisha watu.
Kumekua na majalada kadhaa yanayomuhusu kwa kudhalilisha watu mbalimbali na hakuna hatua yeyote imechukiliwa dhidi yake. Leo Ameenda katika habari yw kumuhusu Askofu na kuandika maneno mabaya na ya kuvunja heshima kwa kiongozi wetu wa Kiroho.
Unapomdharau Askofu ni Umedharau Kanisa, Unapolidharau kanisa ni umedharau waumini wake. Nichukue nafasi hii kuwasihi watu na watumiaji wa mitandao, Kuheshimu viongozi wetu wa dini nila kujali ni wa Dini gani ili mradi amekua kiongozi wa imani ya watu basi waheshimiwe.
Pia nichukue nafasi hii kuvisihi vyombo vya usalama kuchukua hatua ya haraka kwa huyu Rachel Temu kabla hajaafanya kubwa zaidi ya hilo.
Inahitajika hatua za haraka kuweza kudhibiti hili la huyu binti na wengine wenye Tabia kama yake.
Tutalia madhabahuni, na kumlilia Mungu, Kama hatochukiliwa hatua basi Mungu ataamua Hatma ya kinywa kisicho na hekima kwa kiongozi wa Dini.
Mwanakondoo Amezaliwa leoView attachment 2459311