Recipe ya Kauzu wa Kigoma

Recipe ya Kauzu wa Kigoma

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Natafuta Recipe nzuri ya kupika kauzu wa Kigoma; wenye kujua mapishi ya kauzu nisaidieni.
 
Wale jamaa wa mapishi kwenye vipindi vya tv na radio kuna namba huwa wanaziweka ungejaribu kucheki na hao kama huku majibu haupati.
Unaweza kunipa namba zao niwapigiea?
 
Kauzu wa kigoma wanapikwa kwa mafuta ya mawese, kitunguu, nyanya chungu na ndimu.
Umeanza, sasa nipe ukweli wote. Mawese, vitunguu, nyanya chungu na ndimu nitapata tu, wewe nipe ufundi wa kuvichanganya.
 
Sijawahi kuzinakili namba zao.
Ukipata namba ya mmoja wao nitumie haraka sana kwenye pm, nitawapigia. Ninaishi nje ya nchi na majuzi nilipata begi moja la kauzu kutoka Kigoma na natamani sana kuwala ile sijui jinsi ya kuwapika ili niwale.
 
Poa.
 
Umeanza, sasa nipe ukweli wote. Mawese, vitunguu, nyanya chungu na ndimu nitapata tu, wewe nipe ufundi wa kuvichanganya.
Loweka dagaa kwa saa moja na uwaoshe kutoa mchanga. Weka mafua jikoni yakipata moto kaanga vitunguu, vikiwa tayari weka dagaa, malizia na nyanya chungu, ndimu na chumvi.
 
Loweka dagaa kwa saa moja na uwaoshe kutoa mchanga. Weka mafua jikoni yakipata moto kaanga vitunguu, vikiwa tayari weka dagaa, malizia na nyanya chungu, ndimu na chumvi.
Ni rahisi namna hiyo? basi Poa, nitakutumia kadi ya dinner siku mbili zijazo.
 
Kauzu wa Kigoma wanapikwa kwa mafuta ya mawese, kitunguu, nyanya chungu na ndimu.
Ngoja nikuulize swali kidogo; je nisipopata mafuta ya mawese naweza kutumia mafuta ya nazi au ya mzeituni?
 
Sky Eclat naona naanza kuchanganganywa kidogo; hebu nisaidie kwani udenda unaitoka, na sitaki kufanya makosa. Kila ushauri uliondikwa hapa nimeutilia maanani sana. Halafu Da'Vinci , wewe alternative yako ni ipi kabla sijaanza zoezi lenyewe?
Chagua litakalo kupendeza wewe.
 
Back
Top Bottom