The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Si kweli. Machawa hawayajui japo wanayaimba ila hawayatumii. Yote rererere tu! Kwani, wanabomoa, wanapatiliza, si wastahimivu, na mwisho, ni wabomoaji.Reform=mabadiliko
Resilience=ustahimilivu
Reconciliation=kuridhiana
Rebuilding=kujenga Upya
Sasa kumetokea kambi moja inayotumia maneno hayo kama vile ni maneno au tabia yao na wengine wanapata fadhila kwa kupewa maneno hayo.
Suala jingine ambalo ni muhimu kuliko kuyatamka maneno hayo ni kuyaishi.
Reform= mabadiliko naona ina endana na azma ya chama kimoja kinachotaka mabadiliko katika Katiba yetu na tunavyotenda au kuendesha serikali yetu na mengineyo.
Sasa nashanga kuona wanao pigia chapuo maneno hayo kama yao hawayaishi maneno hayo Bali yanatumika katika kuwakandamiza wengine.
Ukija katika neno Resilience au ustahimilivu ni kuvumiliana kwani Binadamu hatufikiri au hatuamini kwenye njia moja, hivyo kila MTU afuate njia yake ili mradi asivuke mstari, akakukanyaga n.k.
Lakini ukija kisiasa na kijamii, viongozi waliopo madarakani na walio nje ya serikali wanatakiwa kuishi kwa pamoja na kukubaliana kwamba kila moja na ana mwenendo wake wa kuongoza ili mradi usivunje Sheria au kutumia Madaraka yako vibaya. Sasa hapa tuwaachie wananchi waamue Nani sio mstahimilivu wa mwenzake.
Reconciliation= kuridhiana ni Nani katika hawa waliopo serikali na wale wasio kwenye madaraka ambaye hataki kuridhiana na mwenzake Kiasi cha kutumia nguvu kumuumiza mwingine.
Neno la mwisho ni rebuilding au kujenga Upya. Je waliopoa madarakani na wasio madarakani ni wapi ambao hawajishughulishi na kujenga Upya kwa mahusiano yetu.
Reform kwao ni deform.
Resilience kwao ni recidivism,
Reconciliation kwao ni retribution.
Na Rebuild kwao ni ruin and rubbish.