Recover The Lost Memory: Kabla ya Kuishi hapa Duniani ulikuwa hai

Kuepuka kufanya makosa, yafaa kufafanua maana ya maneno.

Neno maarifa linatangulia maneno elimu, ujuzi, uzoefu na hekima, ukiacha hekima kutoka kwa Mungu.

Mambo kwa mfano, sayansi ya vitu, elimu kuhusu mtu, matukio, kutokufa kwa roho au nafsi, asili na uwepo wa Mungu, nadharia mbalimbali ni vitu vingi vya maarifa.

Kwa hiyo, maarifa ni tofauti na somo linalojulikana na kitu kinachojulikana.

Elimu sawa na ujuzi sawa na hekima ya binadamu, ni somo linalojulikana na kitu kinachojulikana.
 
Ndugu* unatakiwa uwe tayari kufundishwa. Hapa umeandika maandishi bila hata kueleweka ulichokuwa unataka kuongea. Nakusihi ukae utulie ili uweze kuandika katika mpangilio mzuri.

Kwa faida pana ya watu wengine:

1. Kila mtu anapozaliwa anakuwa na Ufahamu kwa kingereza tunasema Understanding

2. Baada kuwa na Understanding mtu huyo atakuwa tayari kupatiwa Elimu kwa kingereza tunasema Education

3. Atakapoienelewa education (Elimu) aliyopatia anapata Maarifa kwa kingereza tunasema Knowledge. Maarifa ni tunda la elimu. Huwezi ukapata maarifa pasipo kuwa na elimu.

4. Akianza kutumia Maarifa hayo anakuwa amepata Ujuzi kwa Kingereza tunasema Skill. Ujuzi ni tunda linalozaliwa kutokana na Maarifa.

5. Mtu akiutumia ujuzi huo kwa muda mrefu anapata kitu kinachoitwa Uzoefu kwa Kingereza tunaita Experience. Uzoefu ni tunda linalotoka na kutumiza ujuzi mara kwa mara.

6. Baada ya kuwa na Uzoefu kwa kitu hicho kwa muda mrefu na kukitumia kwa namna tofauti tofauti unapata Hekima kwa Kingereza tunaita Wisdom. Hekima ni tunda linalotokana na Uzoefu. Mtoto mdogo anaweza kufanya jambo akaonekana ametenda kwa namna bora. Hiyo siyo Hekima bali ni Busara.

Natumaini umepata kujifunza
 
Hakuna anayejua , ukifikiria sana unaweza kupagawa bure
 
. Kila mtu anapozaliwa anakuwa na Ufahamu kwa kingereza tunasema Understanding

2. Baada kuwa na Understanding mtu huyo atakuwa tayari kupatiwa Elimu kwa kingereza tunasema Education
Nini kinatangulia kati ya maarifa, elimu, ujuzi, hekima na uzoefu? Kipi ni chanzo cha kingine na nini maana ya kila kimoja. That's my question.

Back to your comment.

Sio tu mtu hata wanyama wanapozaliwa wanakuwa na ufahamu.

Maana na tofauti ya elimu, ujuzi, uzoefu, hekima na maarifa ni hii:

Maarifa maana yake ni uwezo wa kufikiri na kufanya uchunguzi kujua ukweli na kujua kuleta vitu vipya kwa kutumia vitu vilivyopo.

Elimu maana yake ni tendo lenye athari ya kujenga akili, tabia na uwezo wa kimaumbile wa mtu.

Elimu anayofundishwa mtoto au mtu nyumbani au chuoni ni maarifa ambayo yaliletwa kupitia kufikiri na kufanya uchunguzi, kujua ukweli.

Aidha, mtu anaweza kutumia elimu aliyofundishwa au aliyojifunza katika kufikiri na kufanya uchunguzi, kujua ukweli na kujua kuumba vitu vipya kutokana na vitu vilivyopo, maarifa.

Ujuzi ni elimu ambayo mtu anajifunza au anafundishwa jinsi ya kufanya kazi fulani au kutoa huduma (know -how). It is a procedural knowledge. Then, it is a subject that is known and a thing that is known.

Hekima - hukumu - haki (wisdom) maana yake ni kujua kuamua bila kukosea. Lakini unawezaje kujua kuamua bila kukosea kama hujui ukweli? Na ukweli utaujuaje?

Uzoefu kwa wenyewe sio maarifa kwa sababu haubebi taarifa zote na unategemea vitu vingi kufikia ukweli.
 
Umeandika maneno meengi nje ya mada. Hebu acha kuchafua vitu visafi.
 
Umeandika maneno meengi nje ya mada. Hebu acha kuchafua vitu visafi.
Huwezi kutoa somo wakati hufafanui misamiati katika hicho unachoita somo.

Vinginevyo unahubiri hisia na uzoefu binafsi ambao ili kuuthibitisha kuwa ni kweli lazima tuangalie vitu vingi.

Umetaja ufahamu lakini hujafafanua ufahamu ni nini. Umetaja elimu hujafafanua elimu ni nini.

Umetaja ujuzi lakini hujafafanua ujuzi ni nini. Umetaja maarifa lakini hujafafanua maarifa ni nini, na uzoefu ni nini.

Umetaja Roho lakini hujafafanua roho ni nini, na nafsi ni nini.

Umetaja ndoto lakini hujasema ndoto ni nini na Lucid dreaming ni nini.

Umetaja ulimwengu lakini hujafafanua ulimwengu ni nini.

Umetaja ulimwengu wa nyama na damu lakini hujafafanua ni nini na ulimwengu wa roho ni nini.

Katika hayo yote unasema unatoa elimu au unafundisha somo! Somo gani unafundisha?
 
Mimi huwa najiuliza msingi wa mwanadamu Unaendeshwa kwa matumaini au akili? vile naona watu wengi wakikosa matumaini hujiua au kujizuru kwa kutumia vilevi nk. Wewe mtoa maada unaonaje hili?
Apo kwenye matumaini(HOPE) mkuu

Mafundisho ya kidini yanatupa matumaini kwamba there is life after death. Vyema sana kuamini na imani ndo inatupa matumaini.
 
kweli kabisa tupo hapa Kama wajinga tu.!
 
Kama yupo huyo muumba basi ana mambo yahovyo tu imagine kamuumba kuku ili akulwe yeye na mayai yake au swala akulwe na simba. mbona uonevu tu.! au nayeye ndo tabia yake.? hata haya mazingira unasema tunahalibu ni yeye kayata tu πŸ˜‚ imagine tungekua na mbawa kusingekua nahaja yakutengeneza gari .! moshi waviwanda ungetoka wapi.?
 

πŸ™„πŸ™„πŸ™„
 
Too short.
 
Ukifuatilia vizuri, humu jamvini huwa kunakuwa na kundi la watu ambao aidha Kwa kukusudia au kutokusudia huzuia watu kutoa Elimu waliyo nayo Kwa wengine...
Hasa pale mtoa mada anapokuwa na roho ndogo ndio huwa hatoboi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…