Juni 15, 2023, Mdau wa JamiiForums aliweka chapisho linaloelezea jinsi alivyokwenda kupata chanjo ya COVID-19 na kupatiwa cheti ya chanjo husika.
Mdau huyu anaeleza kuwa alitishwa sana kabla ya kupata chanjo hiyo na wengine walimuomba alipie tu pesa ili apatiwe cheti kama sehemu ya uthibitisho wa kuchanjwa.
Katika Mjadala huo, mchangiaji mmoja alisema kuwa Taasisi ya Msalaba Mwekundu (Red Cross) ilikuwa imetoa taarifa inayokataza watu waliochanja kuchangia damu kwa wahitaji.
Taarifa hii ni sahihi?
Mdau huyu anaeleza kuwa alitishwa sana kabla ya kupata chanjo hiyo na wengine walimuomba alipie tu pesa ili apatiwe cheti kama sehemu ya uthibitisho wa kuchanjwa.
Katika Mjadala huo, mchangiaji mmoja alisema kuwa Taasisi ya Msalaba Mwekundu (Red Cross) ilikuwa imetoa taarifa inayokataza watu waliochanja kuchangia damu kwa wahitaji.
Taarifa hii ni sahihi?
- Tunachokijua
- COVID-19 au Corona Virusi Disease of 2019 (Ugonjwa wa Virusi vya Korona wa Mwaka 2019) ni Mlipuko wa Kimataifa wa ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vikali vinavyoathiri mfumo wa upumuaji vinavyoitwa coronavirus 2 (SARS-CoV-2).
Visa vya kwanza vya virusi vya corona (nCoV) viligunduliwa kwa mara ya kwanza nchini China mnamo Desemba 2019, huku virusi hivyo vikisambaa kwa kasi katika nchi nyingine duniani kote. Hii ilisababisha Shirika la Afya Duniani (WHO) kutangaza Dharura ya Afya ya Umma inayohitaji Uangalizi wa Kimataifa (PHEIC) mnamo Januari 30, 2020.
Hatua hii ilisababisha kuanzishwa kwa taratibu kadhaa zilizolenga kupambana na usambaaji wa kasi wa ugonjwa huu ikiwemo kunawa maikono kwa sabuni na maji tiririka, kuvaa barakoa, kuepuka misongamano na kupata chanjo ambapo Tanzania kama ilivyo kwa nchi zingine iliamua kuruhusu matumizi ya chanjo kadhaa ikiwemo J&J, Pfizer.
Uhusiano wa Red Cross na uchangiaji Damu
JamiiForums imezungumza na Afisa wa Red Cross Tanzania ili kupata uhusiano wa Taasisi hii na jinsi inavyohusika katika zoezi la Uchangiaji wa Damu nchini.
Afisa huyu ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi amesema kuwa Watu waliopewa haki ya kisheria ya kusimamia ukusanyaji wa Damu nchini ni Mpango wa Taifa wa Damu salama. Red Cross huhamasisha tu uchangiaji lakini haihusiki na ukusanyaji wala utunzaji wa damu hiyo. Amesema;
"Kuna watu ambao wanahusika na mambo ya damu ambao ni Damu Salama, hao ndio huhusika na ukusanyaji wa damu kwa maana hao ndio wameruhusiwa kisheria. Sisi kama Taasisi au Mamlaka tunahamasisha tu au kuandaa yale matukio ambayo tunahamasisha watu wachangie. Kwa hiyo labda katika kuhamaisha kwetu lazima hao watu wa damu salama wawe na taarifa na wawepo sababu wao ndio wanahusika na ukusanyaji pamoja na utunzaji wake, sisi tukimaliza hapo inakuwa imeisha"
Red Cross wamezuia watu waliochanja kuchangia Damu?
JamiiForums ilitaka pia kufahamu kama Taasisi hiyo imekataza watu waliopata chanjo za UVIKO-19 kuchangia damu kama ilivyodaiwa na mdau. Afisa huyo anaendelea kufafanua;
"Haina Madhara yoyote mpaka sasa hamna mtu aliyekatazwa, kwa sababu hiyo inaruhusiwa kwa sababu hadi sasa asilimia kubwa ya watanzania wamechanjwa na zoezi hilo (la ukusanyaji Damu) linaendelea. Mpaka sasa hatuna taarifa kama kuna katazo lolote"
Amebianisha kuwa mtu yeyote mwenye afya nzuri anaweza kuchangia damu kwa kufuata vigezo maalumu vilivyowekwa na wataalamu wa afya.
Kazi za Red Cross
Kulingana na Sheria ya Uanzishwaji wake, Red Cross ni taasisi inayosaidia Serikali kwenye majanga ya aina mbalimbali ikiwemo njaa, mafuriko, magonjwa ya mlipuko, huduma ya kwanza n.k
JamiiForums imebaini kuwa wahusika wakuu wanaoratibu Utaratibu wa chanjo Tanzania ni Wizara ya Afya na sio Red Cross kama ambayo taarifa zinavyodai hivyo wenye Wajibu wa kutoa tahadhari ni Serikali kupitia Wizara hiyo.
Maombi ya kupata chanjo hii hufanyika kupitia tovuti Rasmi ya Serikali ilivyo chini ya Wizara ya Afya ambapo waombaji hupaswa kujaza taarifa zao kisha kupata kituo husika kwa ajili ya chanjo.
Red Cross haihusiki kwa namna yoyote kwenye kuratibu utoaji wa Chanjo za COVID-19 hivyo isingeweza kutoa tamko lililo nje ya majukumu ya msingi ya kuanzishwa kwake.