Uchaguzi 2020 REDET kutoa Taarifa ya Utafiti kesho?

Uchaguzi 2020 REDET kutoa Taarifa ya Utafiti kesho?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Kuna Taarifa zinazunguuka mitandaoni kuwa REDET wanajipanga kutoa ripoti ya utafiti wa mwenendo wa kisiasa nchini kesho tarehe 27/10/2020.

Kama REDET watatoa taarifa hizo wakati nchi inaingia kwenye uchaguzi wa rais na wabunge siku ya pili yake itakuwa ni ubakaji wa hali ya juu ya tasnia ya utafiti nchini kwa maana kwa vyovyote vile itakuwa ni mchezo wa kujaribu kutumia Utafiti kwa ajili ya kutumika kisiasa.

Namuonya Profesa Mukandara kuwa heshima yake kama mwanataaluma nguli, na mtafiti mwenye kuheshimika, heshima yake itaingia doa sana hadi kuchafuka asikoweza kujisafisha kama atashiriki mchezo huo mchafu!

Profesa ajue tu kuwa dunia ya leo ni kijiji na tekinolojua iko wazi, Kama akifanya mchezo huo jumuia ya wasomi wenzie watamdharau sana na heshima yake aliyoijenga kwa muda mrefu itashuka kwa kiwango kisicho mithilika. Na tutasambaza utafiti wake huo katika taasisi mbalimbali duniani wakiwemo "wadau wa maendeleo wa Taasisi hiyo" ili waone hiyo Taasisi ilivyo kituko!

Nawaomba watu wa REDET kama mnapanga kutumika ili kubadili public opinion, au kujustify uporaji wa haki za wananchi basi acheni, hatutowasamehe! Taifa na sauti za wananchi ni bora kuliko vijisenti viwili vitatu au vyeo vya hapa na pale!

Watanzania tuko macho, tunafuatilia sana. Attempt yoyote au Utafiti wowote utakaotoka kukiwa kumebaki Siku moja ili kupiga kura, Hiyo ni Professorial rubbish, na wala hatutaichukulia serious, na yeyote atakayehusika kuleta ufiti huo kanjanja basi tunajua tu kuwa anatumika na tutamdharau na kumpuuza bila kujali kiwango chake cha elimu ya makaratasini. Msomi wa kweli hawezi kukubali kutumika na wanasiasa!, Huyo ni msomi Kanjanja na Feki.

Utatoaje taarifa za utafiti wakati katika sehemu moja ya muungano yaani huko Zanzibar watu wameanza kupiga kura siku hiyo? huo ni ukhanithi wa kitaaluma!
 
Kuna Taarifa zinazunguuka mitandaoni kuwa REDET wanajipanga kutoa ripoti ya utafiti wa mwenendo wa kisiasa nchini kesho tarehe 27/10/2020...
Sasa unamuonya kivipi,si huyo jamaa yenu mwenye mashavu makubwa anauhakika wa kushinda urais ,huoni kuwa huo utafiti lazima uoneshe lissu kibaraka wa mabeberu atashinda kwa asilimia 99.999 kwahiyo itamrahisishia kuingia ikulu ya chamwino
 
Hahahhaa Jamaa unaogopa nini unakataza watu kutimiza wajibu waoo hahah Tulieni
 
Kila chama kinajua ukubalika wake - mie ningetoa takwimu za mwanza, geita, kagera na kigoma lkn kwa kuwa sina kibali nakaa kimya

Kura za Urais kutakuwa na kuzidiana kwa asilimia zisizozidi 5% (48.7 kwa 49.1) na 2.2 kwa vyama vingine
 
Kuna Taarifa zinazunguuka mitandaoni kuwa REDET wanajipanga kutoa ripoti ya utafiti wa mwenendo wa kisiasa nchini kesho tarehe 27/10/2020.

Kama REDET watatoa taarifa hizo wakati nchi inaingia kwenye uchaguzi wa rais na wabunge siku ya pili yake itakuwa ni ubakaji wa hali ya juu ya tasnia ya utafiti nchini kwa maana kwa vyovyote vile itakuwa ni mchezo wa kujaribu kutumia Utafiti kwa ajili ya kutumika kisiasa...
Paid agents have to be ignored. They want to justify the mischief planned by NECccm.
 
Heshima ya Profesa Mukandara iko hatarini kuingia kwenye shimo la taka

Profesa awe makini asitumike, atadharaulika sana!
 
Mbona mnatanguliza denials? Mbona mnakuwa na mashaka na kila taasisi?

Hujui humo Kuna Nini halafu Bado unalalamika [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Makamanda gwanda zishalowa tayari kwa doso[emoji23][emoji23]
 
CCM siyo mbaya tatizo wanaotawala salama hawana huruma na binadamu
 
Back
Top Bottom