Redio maria acheni udini, nyie kutwa kutwa mambo ya dini ya ukristo na kwaya tu?

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,079
Reaction score
2,947
Radio maria acheni udini aisee mnazingua aisee Tanzania kuna dini kubwa mbili aisee sasa kwanini kila siku nyie mnaizungumzia dini moja tu ya ukristo? Ili hali nyie ni radio tu kila mtu anapaswa kuisikiliza sio kubase kwenye dini moja tu aisee mnakera sana aisee

Mtanirekebisha kama ni radio ya dini maana sijajua aisee kwasababu leo ndio nimeisikiliza nikiwa kwenye daladala! Mtanirekebisha aisee
 
Tangu lini bucha la halal likauza kitimoto. Jifunze kuheshimu taasisi za watu.

Ni sawa na kusema Kila simu msikitini wanahubiri hadith za Mtume Mohammad SAW. Basi siku Moja Moja wawe wanamhubiri Kristo. Haiwezekani.

Nilifikiri ungewasema TBC kwa nini Kila siku wanawasemea CCM TU, ningekuelewa
 
Si mna TV imaan mnaacha inajifia unatamani radio Maria inayoendeshwa kwa sadaka za waumini wao wawaenezee dini yenu? Nyie watu ni misplaced organism.... mnashangaza sana!
 
Fungua ya kwako hao wa dini waachie redio Yao!
 
Kuna ule uzi wa jamaa alisema Radio Imaan ina watangazaji wachache wadau wakadai hata shift hao hawapeei na kuna ukata wa fedha waumini wagumu kuchangia.
 
Reactions: K11
Kwahiyo unataka waanze kuweka kaswida na kuwaita waganga wa tiba za kusuni waje kutangaza dawa zao mle?
 
Sasa ulitaka wapige qaswida ama
 
Watu bana. Unajua malengo ya kuanzishwa kwake au unabwabwaja tu siku iende.
 
Mtanirekebisha kama ni radio ya dini maana sijajua aisee kwasababu leo ndio nimeisikiliza nikiwa kwenye daladala! Mtanirekebisha aisee
Kila jambo huanzishwa kwa kusudi lake,
Radio Maria ilianzishwa mahususi kwa ajili ya uinjilishaji, ni km Radio Imani ilivyoanzishwa kwa ajili ya kuwajenga waislam kiimani!
Zipo Radio nyingi unaeza kusikiliza sawa na mahitaji yako, Jielekeze huko!!
 
Hii ni ya Njombe sio ya Arusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…