Mkuu mashabiki wengi wa mpira hapa bongo Ni wanafiki tu. Kuna matukio mengi yameishatokea kwenye Michezo iliyotangulia especially Simba sc Ila hatukuona kelele Kama wanavyopiga kwa tukio la Jana ambalo kimsingi upande wangu naona matukio ya kawaida kwenye viwanja vyetu. Mojawapo Ni Hilo la Kennedy Juma kumkita maksudi mchezaji wa Biashara United mgongoni Tena akiwa Hana mpira watu mkakaa kimyaaa Kama Hakuna lililotokea. Kama tunataka kuwa fair Basi tusiwe bias hapo ndipo kelele zetu zitakuwa na maana. Namalizia kwa kusema Jana Namungo wa walituzidi, penalty ya Yanga Ni halali nimeangalia Mara kadhaa, Ila mazingira ya kupiga penality ndiyo hayakuwa halali maana wachezaji kadhaa walikuwa kwenye box pamoja na mwamuzi. Mechi imeisha hiyo tujipange kwa matukio mengine kwenye mechi zijazo.