Hakuna cha figisu hapo acheni kulalamika bwana, anaejua mpira anajua tu wala hahitaji nguvu kubwa ni akili na maarifa zinatumika uwanjani, wenzetu wametuzidi mbali sana. Nimetazama 90 minutes sijaona figisu yoyote, refa amechezesha kwa umakini bila kuegemea pande yoyote,, na mazembe walizidiwa mwanzo mwisho, acheni kulalamika, daima zikikutana timu za waarabu na west or south na zikafungwa mnaanza malalamishi mara oh wamebebwa, refa amepewa mpunga, oh figisu nyingi, hebu tuacheni uswahili uswahili wa uyanga na usimba bwana.
Ball possession zinaongea, total shots zinaongea, chances created zinaongea, big chences zinaongea, accurate passes zinaongea, pass success zinaongea, corners zinaongea, on targets zinaongea, passes zinaongea, mnscholslamikia nini!!! haya weka na mazembe yako hapa tuone, maana huko kwao waliambulia goli moja tena kwa mbinde, home away wamepigwa 4G, hapo nani kaonyesha ukubwa?
Ubaguzi bado unalitesa bara letu, na ndio maana soka letu haliendelei,, wenzetu wanaendelea kusonga mbele, sisi maneno mengi vitendo zero.
Kuhusu kombe la dunia, hao unaotumia nguvu kubwa kuwatetea bila mantiki yoyote wamefanya nini kombe la dunia! Atleast Algeria alijitahidi 2014 dhidi ya ujerumani, alimkazia mpaka dakika 90, wakaongezwa na mpira ukaisha kwa 2-1. Hao wengine walifika wapi?
Tuacheni ubaguzi ndugu hata kama kuwachukia sio hivyo tena babaa,, na usijitoe ufahamu kilichotokea kwa egypt dhidi ya senegal, Algeria dhidi ya Cameroon kila mtu aliona na kushuhudia matukio yaliyotokea mpaka aibu.
Nachukia sana ubaguzi.