Refa Asimamisha Mechi, Akojoa Live Uwanjani

Nyundo_tz

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2009
Posts
640
Reaction score
20
Friday, September 25, 2009

Refa aliyekuwa akichezesha mechi ya ligi kuu ya Qatar alitoa kali ya mwaka ambayo haijawahi kutokea kwa kusimamisha mechi kwa muda na kuanza kukojoa katikati ya uwanja huku televisheni za nchi hiyo zikirusha Live mechi hiyo.

Refa huyo alikuwa akichezesha mechi ya ligi kuu ya Qatar kati ya timu ya Al Gharafah na Al Khor ambayo wenyeji Al Gharafah walishinda kwa mabao 4-1.

Tukio hilo la aina yake lilitokea katika kipindi cha pili cha mechi hiyo iliyochezwa majira ya usiku wakati refa huyo alipomzuia mchezaji asipige kona kwanza ili aweze kujisaidia uwanjani.

Wakati wachezaji wakisubiria refa aamuru kona ipigwe, refa huyo akiwa amesimama ndani ya boksi la 18, alishusha bukta yake na kuanza kukojoa wazi wazi uwanjani.

Televisheni za Qatar zilinasa tukio live lakini zilishindwa kulionyesha wazi na kuamua kuweka kiboksi cheusi kuzunguka maeneo ya siri ya refa huyo.

Baada ya kumaliza kujisaidia refa huyo aliamuru kona ipigwe na mechi iliendelea kama kawaida.
 
bora imetokea huko qatar maana ingekuwa hapa kwetu ingehusishwa na uchawi....................na timu ambayo inefungwa ingekata rufaa si unajua yale mambo yetu
 
hahahahaha..... hii kiboko nimecheka hdi mbavu vinauma
 
bora imetokea huko qatar maana ingekuwa hapa kwetu ingehusishwa na uchawi....................na timu ambayo inefungwa ingekata rufaa si unajua yale mambo yetu
Uko ryt mkuu, maana hapa hata ukiongea na refa uwanjani tayari deal.
 
kwani kipindi cha mapunziko alikuwa anafanyanini... marefa wetu bongo mwaionaje hii na shirikisho la soka FIFA linasemaje kuhusiana na hiii....
Sipati picha angekuwa refa wa kike ingekuwaje.....
 
Hahahahaha dah hii kiboko kwa hiyo jamaa alibanwa mno nn?
 
Hahahahaha dah hii kiboko kwa hiyo jamaa alibanwa mno nn?

Inawezekana ana mashine kubwa akataka aiweke hadharani. Angekuwa na kaduchu asingethubutu kukamwaga hadharani.
 
Siku hizi huwezi danganya watu kirahisi, ngoja nivute picha
 
Video
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=VuhaLjiiJQc[/ame]




 

Attachments

  • ref taking a leak_v2.jpg
    14.4 KB · Views: 198
Duh hii nayo inapendeza, mwishowe watajisadia na kubwa
 
Bora kuchekesha watu kuliko kupata madhara ya kibofu
 
Huko Qatar, wadada hawaruhusiwi kwenda kwenye futiboli, ndio maana refa huyo kafanya alivyofanya
 
huyu refa kiboko lakini jamani kama alizidiwa angefanyaje mwenzenu?
 
kwani kipindi cha mapunziko alikuwa anafanyanini... marefa wetu bongo mwaionaje hii na shirikisho la soka FIFA linasemaje kuhusiana na hiii....
Sipati picha angekuwa refa wa kike ingekuwaje.....

Hayo yashamkuta Lucas Radebe wakati anachezea Leeds, yeye alipatwa na haja kubwa katikati ya mchezo ikabidi aende kujisaidia, alipomaliza haja yake anakuta wenzake washalala moja bila!!!!!
 
Ungekua wewe ndio huyo refa na umebanwa na mkojo uwanjani ungefanyaje?
Ngoja tusikie shrikisho la soka la QUATAR juu ya hatua waliyomchukulia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…