Nyundo_tz
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 640
- 20
Friday, September 25, 2009
Refa aliyekuwa akichezesha mechi ya ligi kuu ya Qatar alitoa kali ya mwaka ambayo haijawahi kutokea kwa kusimamisha mechi kwa muda na kuanza kukojoa katikati ya uwanja huku televisheni za nchi hiyo zikirusha Live mechi hiyo.
Refa huyo alikuwa akichezesha mechi ya ligi kuu ya Qatar kati ya timu ya Al Gharafah na Al Khor ambayo wenyeji Al Gharafah walishinda kwa mabao 4-1.
Tukio hilo la aina yake lilitokea katika kipindi cha pili cha mechi hiyo iliyochezwa majira ya usiku wakati refa huyo alipomzuia mchezaji asipige kona kwanza ili aweze kujisaidia uwanjani.
Wakati wachezaji wakisubiria refa aamuru kona ipigwe, refa huyo akiwa amesimama ndani ya boksi la 18, alishusha bukta yake na kuanza kukojoa wazi wazi uwanjani.
Televisheni za Qatar zilinasa tukio live lakini zilishindwa kulionyesha wazi na kuamua kuweka kiboksi cheusi kuzunguka maeneo ya siri ya refa huyo.
Baada ya kumaliza kujisaidia refa huyo aliamuru kona ipigwe na mechi iliendelea kama kawaida.