Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Wakati tunaenda kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mwingine ni vizuri tukaangalia nyuma na kujifunza kwa waliyopita. Moja ya kitu nilichoona hiki, watu wengi tumebeba trauma za utotoni na kufanya haya ndio yawe maisha wetu. Mtoto anajifunza kwa kuiga kutoka kwa waliomlea na wanaomzuka, wewe wa leo pamoja na matendo yako ni zao la ulichobeba kutoka kwenye makuzi yako iwe baya au zuri
Ulikuwa abused ukiwa mtoto na hukupata nafasi ya kusema sasa umekuwa mkubwa ama unaendeza abuse hizo kwa watu wengine, au unakubali kufanyiwa abuse na kukubali kuwa haya ndio maisha, uliambiwa hutakiwi kujiweka mbele unatakiwa uangalie wengine kwanza sasa hivi umekuwa hajijali kabisa, self love ni msamiati mgeni kwako, hujui kusema hapana, unatumika mpaka unaisha lakini hujawahi kujihudumia wewe kabisa sababu unaamini kufanya hivyo ni kuwa selfish.
Uliambiwa wewe ni useless huwezi kufanikisha kitu, leo umekuwa unashindwa kufata ndoto zako sababu ndani sauti inakwambia wewe ni useless na utashindwa tu, hukupata upendo wa baba/mama leo umekuwa mtu mzima unafanya hivyo hivyo kwa watoto wako, akilini ukijua huo ndio mtindo wa maisha watoto inabidi wawe ngangari unazidi kutengeneza matatizo zaidi, maisha yako yote umeona baba/mama yako akinyanyaswa sana kwa kipigo au kihisia mpaka siku anafariki hakuwahi kulalamika au kuomba msaada nawe leo umekua unaishi maisha haya haya, imekuwa kawaida, unashindwa kuomba msaada au ku walk away, nk, nk.
Vivyo hivyo kama wanaokuzunguka walikuwa wanaishi kwa upendo, kuheshimiana, kusaidiana, kujipenda, navyo vitareflect kwako leo wewe ni mtu mzima.
Baadhi tumetambua tuna vidonda vya nyuma vinavyohitaji kushughulikiwa ili tuishi maisha ya furaha na kufikia potential zetu, lakini wengi wetu bado hii ni changamoto kubwa. Hatujawahi hata siku moja kukaa chini na kureflect jinsi maisha yetu yalivyokuwa utotoni, je uliteendewa sawa, waliokuwa wanakuzunguka ambao ndio walikuwa kioo chako walikuwa wanakufundisha nini? Leo umekuwa unaishije? Unawatendea vipi wanaokuzunguka? Unajitendea vipi wewe mwenyewe? Je hivyo ndivyo unavyotakiwa kuishi?
Baada ya kujiuliza maswali hayo utajua trauma zako ziko wapi ili uzifanyie kazi. Process hiyo haitamalizika siku moja tu kwamba unaamka leo umepona kila kitu, lakini kutambua kwamba nafanya hivi kutokana na trauma hii ni hatua nzuri ya kuweza kuanza kufanyia kazi na ku act right.
Process haitakuwa rahisi, don't be hard on yourself uchukue hatua moja kila siku, siku nyingine utalia sana urevisit your old self ili kujiponya, ila kadri siku zinavyoenda utazidi kujitambua na hatimaye kupona kabisa. Kaone mwanasaikolojia kama huoni pa ku kuanzia, hawapo kwaajili ya watu waliochanganyikiwa tu, ili upate msaada stahiki.
Narudisha kijiti kwenu wakuu, kutokana mada hii umeona chochote unachofanya sasa ambacho unaona kabisa ni kutokana na trauma ya utotoni? Utafanya nini kudeal na hilo? Reflection nyingine umefanya wakati huu?